Afisa afya wilaya ya Makete Bw. Abraham Sanga(kulia) akizungumza kuhusu hali ya lishe katika studio za Kitulo Fm, kushoto ni mtangazaji wa kipindi Ergon Sanga.
======
Imeelezwa
kuwa wilaya ya Makete mkoani Njombe ni miongoni mwa wilaya zenye
matatizo ya lishe ambapo kwa mujibu wa utafiti imeonesha kuwa asilimia
60 ya watoto wilayani humo wamedumaa
Kauli
hiyo imesemwa na Afisa lishe wilaya ya Makete Bw. Abraham Sanga wakati
akizungumzia hali ya lishe katika wilaya ya Makete katika kipindi cha
maisha ni afya kinachorusha na redio ya jamii Kitulo Fm iliyopo wilayani
humo
Amesema
utafiti huo ulifanywa kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya
Makete januari 2013 kwa kushirikiana na taasisi ya chakula na lishe
(TFDA), na UNICEF ambapo imegundulika hali ya lishe wilaya ya Maketi si
ya kuridhisha
Bw.
Sanga amesema sababu ya watoto wengi kudumaa ni kuwa huanzia tangu
tumboni kutokana na sababu ya ukosefu wa chakula bora muda mrefu hasa
kwa wajawazito, ambapo amesisitiza ni vyema kwa wazazi kuhakikisha
chakula bora kinapatikana kwa familia ili kuepukana na matatizo hayo
Pamoja
na hali ya udumavu pia Bw. Sanga amezungumzia suala la ukondefu pamoja
na umuhimu wa vitamini A mwilini kwa kuwa vitamini hiyo ni muhimu na
inatumika kusaidia vitu vingi mwilini ikiwemo hali ya kuona vizuri hasa
usiku, taifa kuwa na watoto wenye uwezo mzuri kiakili n.k
Miongoni mwa vyakula vinavyosababisha
mtu kuwa na vitamini A kwa wingi ni mboga za majani kama mchicha,
sukumawiki, tembele, majani ya maboga na pia ziwe za kijani kibichi na zisipikwe zikaiva sana
credit EDDY BLOG