Pichani ni diwani wa kata ya Mjimwema Makambako Bwana Alimwimike Sahwi Akizungumza na Mtandao Huu.
Na Gabriel Kilamlya Makambako
Rai Hiyo Imetolewa na Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Halmashauri Hiyo Wakati Wakiongea na gabrielkilamlya.blogspot.com na Kusema Kuwa Baadhi ya Kata ni Kubwa na Wingi wa Watu Hivyo Bajeti Zinazotengwa Kwa Kata Hizo Hazitoshelezi Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Ikilinganishwa na Kata Nyingine Ambazo Zina Idadi Ndogo ya Watu na Maeneo Madogo.
Miongoni Mwa Wajumbe Waliotoa Rai Hiyo ni Diwani wa Kata ya Mjimwema-Makambako Alimwimike Sahwi Ambaye Ameeleza Kuwa Kata Yake Inakabiliwa Changamoto ya
Bajeti Ndogo Ikilinganishwa na Idada ya Watu na Ukubwa wa Kata ya Mjimwema Hali Inayosababisha Huduma za Kijamii Zinazotolewa Katika Kata Hiyo Kuwa Chini ya Kiwango.
Aidha Diwani Sahwi Amependekeza Kugawanywa Kwa Kata ya Mjimwema na Kuwa Kata Mbili Ili Kusogeza Huduma za Kiutawala na Kijamii Karibu na Wananchi Kutokana na Kata Hiyo Kuwa na Idadi Kubwa ya Watu Pamoja na Eneo Kubwa Kiutawala.
Hata Hivyo Diwani Sahwi Ameipongeza Serikali Kwa Kuipa Kipaumbele Kata Hiyo Katika
Mradi wa Ujenzi wa Barabara Zilizomo Ndani ya Kata ya Mjimwema
Ambapo Takribani Kilomita 49 Zitatengenezwa na Kwamba Tayari Wakandarasi Wamesaini
Mikataba ya Ujenzi wa Barabara Hizo.
0 comments:
Post a Comment