Mkuu wa
wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi akiwahutubia wananchi wa
kijiji cha Mdandu wakati akizindua Chanjo Mpya za watoto za Nimonia na
Kuhara leo.
Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Dr. Conrade Ugonile Katikati akiwa na diwani wa kata ya Mdandu Annaupendo Gombela kulia wakati wa uzinduzi wa Chanjo mpya za watoto
Wananchi wa kijiji cha Mdandu wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo leo.
Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Dr. Conrade Ugonile Katikati akiwa na diwani wa kata ya Mdandu Annaupendo Gombela kulia wakati wa uzinduzi wa Chanjo mpya za watoto
Wananchi wa kijiji cha Mdandu wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo leo.
.......................................................................................................
Zaidi ya Watoto Elfu Kumi Wenye Umri Chini ya Mwaka Mmoja wa Wilaya za
Njombe , Wanging'ombe na Halmashauri ya Mji wa Makambako Wanatarajia
Kupatiwa Chanjo ya Kuzuia Magonjwa ya Nimonia na Kuhara.
Takwimu Hizo Zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi. Esterina
Kilasi Hii Leo Wakati Akizindua Chanjo Dhidi Magonjwa ya Nimonia na
Kuhara Kwa Watoto Waliochini ya Mwaka Mmoja Katika Kijiji cha Mdandu Kwa
Wilaya za Wanging'ombe, Njombe na Halmashauri ya Makambako.
Akizungumza Kwenye Uzinduzi Huo Mkuu Huyo wa Wilaya Amewataka Wazazi na
Walezi Kuwapeleka Watoto Wao Kupatiwa Chanjo Hizo na Kuondokana na Imani
Potofu Zilizojengeka Kwa Baadhi ya Wananchi na Kwamba Chanjo Hizo
Zinalenga Kupunguza Vifo Vya Watoto Waliochini ya Umri wa Miaka Mitano.
Kwa Upande Wake Kaimu Afisa Tarafa wa Mdandu Bwana Benson Wandelage
Amewataka Wazazi na Walezi wa Tarafa Hiyo Kuendelea Kuwapeleka Watoto Wao
Kwenye Vituo Vinavyotolea Chanjo Hizo.
zoezi la Uzinduzi wa chanjo hizo katika halmashauri ya wilaya ya Njombe
limekuja ikiwa ni siku nne tangu halmashauri ya mji wa Njombe kuzindua
chanjo hizo katika zahanati ya Idundilanga Mjini hapa.
0 comments:
Post a Comment