Mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha amewataka watumishi wa
Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kufanya kazi kwa upendo na
mshikamano kama njia ya kuuanza mwaka mpya wa 2013 kwa upendo na
ufanisi zaidi.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli
hiyo leo wakati wa kuwaaga watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa
na kuwakaribisha watumishi wapya pamoja na kuaga na kukaribisha mwaka
mpya wa 2013 ,sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya
wilaya ya Ludewa .
Asema kuwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ni watumishi
ambao wanaweza kulikomboa Taifa katika dimbwi la umasikini iwapo
kama kila mtumishi atadumisha umoja na mshikamano .
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kila mtumishi ni lazima kujuwa
wajibu wake na kutambua malengo yake katika kuitumikia Halmashauri
hiyo ya wilaya ya Ludewa na kudai kuwa baada ya kugawanywa mkoa wa
Iringa na Njombe hivi sasa mkoa wa Njombe ndio unapiga hatua zaidi
katika maendeleo ukilinganisha na mkoa wa Iringa.
Aidha awataka watumishi wa Halmashauri ya Ludewa kuhakikisha
wanafika kazini saa mmoja asubuhi na saa 1.30 kuanza kazi ya serikali
badala ya kufika kazini kwa kuchelewa .
Madaha alisema kuwa hakuna haki bila kutimiza wajibu na kuwataka
watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kutimiza wajibu
kwanza katika kazi badala ya kudai haki bila kutimiza wajibu .
Amtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Fidelis Lumato
kuhakikisha anawabana watumishi wasiowajibika huku akiwataka
watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuzingatia sheria ,kanuni na
utaratibu huku kuonyesha mfano mwema katika maeneo yao ya kazi.
Madaha alisema kuwa hatakuwa na huruma kwa mtumishi wa Halmashauri
hiyo atakayeshindwa kutimiza wajibu wake na kuwa kwa mwaka 2013
nyaraka zote za sheria za utumishi wa umma zitawekwa mahali ambapo kila
mtumishi ataweza kusoma na kuzitambua zaidi ili pale anapokiuka
kuwajibika kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu.
Akemea vitendo vya rushwa katika maeneo ya kazi na kutaka watumishi
kuchukua hatua ya kupambana na rushwa na kuwa rushwa katika wilaya ya
Ludewa inapaswa kupigwa viti na kila mmoja .
Mkuu huyo wilaya amesema kuwa iwapo kila mtumishi wa wilaya hiyo
atafanya kazi kwa uaminifu na kuchukia vitendo vya rushwa wilaya hiyo
itaendelea kupiga hatua katika maendeleo.
Kuhusu wastaafu mkuu huyo wa wilaya alitaka Halmashauri ya wilaya
ya Ludewa kuweka utaratibu wa kuwasaidia wastaafu ili nao waweze
kuendelea na kunufaika na matunda ya Taifa
Alisema kuwa pamoja na wazee wastaafu kulitumikia vema Taifa ila bado
maadili ya Taifa yameendelea kumomonyoka kutokana na wazee
kushindwa kuwafunza vema vijana katika maadili mema na kuwa wazee
waliowengi wanashindwa kuwalea watoto wao katika maadili kutokana na
hali ya umasikini inayowakabili.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akitoa
salam zake katika sherehe hizo alisema kuwa kwa upande wake
amefarijika kufika katika sherehe hizo na kufanya sherehe hiyo ya
kufunga mwaka na watumishi hao huku akieleza matumaini yake makubwa
katika kuwatumikia wananchi wa jimbo la Ludewa .
0 comments:
Post a Comment