Katika hali isiyo ya kawaida shule ya msingi Madeke Wilayni Njombe imekutwa haina hata mwalimu mmoja na vilanja wakikabidhi kuwaongoza wanafunzi wenzao.
Hali hiyo imetokea katika shule hiyo ya madeke wakati mkuu wa wilaya ya
Njombe Bi.Sarah Dumba akifanya ziara ya kutembelea shule za wilaya ya Njombe na kisha kubaini tatizo hilo.
Aidha amese amesema alipofika shuleni hapo hakumkuta mwalimu yeyote zaidi ya mandishi yaliyoandikwa na mwalimu mkuu kuwa yeye anakwenda mjini na hivyo shule kuwakabidhi vilanja.
Kufuatia sakata hilo mkuu wa wilaya ya Njombe amewaagiza walimu kutekeleza majukumu yao na si kuendelea kuilalamikia serikali kutaka kuwatekelezea stahiki zao wakati wao hawatekelezi.Kutokana na hali hiyo mtandao huu wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com umelazimika kumtafuata mwalimu mkuu wa shule hiyo bwana Josephat Mbugi aliyekutwa mjini Njombe kama maandishi yake yalivyoachwa shuleni hapo na kisha kukiri wazi kuwa tatizo hilo limetokana na utoro wa walimu.
Mwalimu mkuu huyo bwana Mbugi amesema kuwa hatua ya kuwaachia wanafunzi kuongoza shule hiyo imetokana na
yeye kubaki pekee yake na hivyo kujikuta akishindwa kutekeleza majukumu yote kwa wakati mmoja na hivyo kuwakabidhi vilanja kuwaongoza wenzao.
Ameongeza kuwa shule hiyo ina jumla walimu wanne na wanafunzi 102 ambapo hadi sasa walimu hao wametoroka na mmoja amesimamishwa kazi kwa sababu ambazo hazikufahamika mara moja.
Kijiji cha Madeke ni miongoni mwa vijiji vilivyopo kata ya Mfiriga na kikiwa mpakani mwa mkoa wa Njombe na Morogoro huku ikitajwa kuwa walimu wanaopelekwa kufundisha shule hiyo ni wale walioshindikana katika maeneo mengine na hivyo kupelekwa kama adhabu.
Pamoja na mambo mengine lakini pia imetajwa kuwa hadi sasa wanafunzi hawapati chakula cha mchana kutokana na kile kinachodaiwa wazazi kushindwa kuchangia chakula licha ya kuchangia fedha kwa mahitaji mengine "alisema
0 comments:
Post a Comment