tg

Monday, February 3, 2014

JESHI LA POLISI MKOANI NJOMBE LATHIBITISHA KUUNGUA KWA BWENI

 
 baadhi  ya wanafunzi wakiendelea kuhamisha moja ya vifaa katika shule hiyo 
 
na picha nyingine ni  moja ya chmba kilichoweza kuungua

Na James Festo, Njombe


Jeshi La Polisi Mkoani Njombe limethibitisha kutokea kwa matukio manne likiwemo la kuungua kwa bweni  katika   shule ya sekondari  ya  Njombe , Watu  watatu kufa kwa matukio mbalimbali likiwemo la kujinyonga na  ajali za barabarani. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Na kusainiwa na kamanda wa polisi   mkoa wa Njomnbe  SACP Fulgence  Ngonyani   imesema kuwa tukio hilo la kuungua kwa bweni hilo katika Shule Ya Sekondari Lilitokea   Tarehe  Mosi  Mwezi  Huu  Majira Ya Saa  12 na Nusu Jioni   Katika Bweni la Wavulana  Namba Saba Ambapo Moto huo Ulizuka katika Bweni  na Kuunguza   Vifaa Mbalimbali Vikiwemo  Magodoro, Mabegi ya Nguo,   Masanduku ya vitabu Vya Wanafunzi 42 Waliokuwa Wakilala Katika Bweni Hilo. 

Hata hivyo taarifa hiyo Ya jeshi La polisi  imesema kuwa   thamani ya mali  mali zote zilizoteketea kwa moto bado haijajulikana  na hakuna madhara yoyote yaliyoweza kujitokeza kwa binadamu na chanzo cha moto huo ilikuwa ni hitilafu ya umeme

Katika tukio jingine   mkazi mmoja wa kijiji cha Uhenga  kata ya Saja  Wilayani Wanging'ombe aliyekuwa Akijulikana  kwa jina la Waidu Lupenza ( 70) alikutwa amejinyonga tarehe mosi mwezi fubruali mwaka huu majira ya saa  12 kamili jioni kwa kutumia khanga  ambapo alikutwa akiwa amening'inia  kwenye kenchi chumbani mwake

Na inasadikiwa  marehemu  alikuwa  anasumbuliwa  na kichwa pamoja na ugonjwa wa maralia  na alijinyonga  mara baada ya  mke wake  aitwaye  Grace  Kivigili  ( 50 )kuenda kutafuta dawa  kwa ajili ya kumsaidia   mume wake  aidha taarifa hiyo imesema kuwa   marehemu hakuacha ujumbe wowote  na chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.


Taarifa hiyo pia imethibitisha kutokea kwa tukio la mauaji  ya Getrude Kaduma  mwenye umri wa miaka 30 katika kijiji cha  Nyamande kata ya Kitandililo  Mkoani Njombe  ambaye alikutwa amekufa shambani mwake  kwa kunyongwa  shingoni  na mtu au watu wasiofahamika

Pamoja na mambo Mengine  pia taarifa hiyo imefafanua kuwa  marehemu katika tukio hilo alibakwa kabla ya kuuwawa  huku chanzo cha tukio hilo  bado kinachunguzwa  na watuhumiwa watatu wamekamatwa  kuhusiana na tukio hilo.

Aidha katika tukuo jingine   mtu mmoja asiyefahamika  na anayekadiliwa kuwa Na umri wa miaka 35 hadi 40  amafariki dunia  tarehe  mbili  mwezi februali mwaka huu majira ya saa mbili na nusu usiku  mara baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T339 AKH aina Toyota Mark II mali ya Aloyce  Mtege  (45) katika maeneo ya Mjimwema na kata ya Mjimwema  Mkoani Njombe 

Tukio hilo ambalo  lilitokea kwenye  barabara ya songea hadi Njombe  na kumsababishia kifo  mtu huyo   na mtuhuimiwa katika tukio hilo anashikiliwa na jeshi hilo Huku  chanzo cha ajali hiyo  bado kinachunguzwa. 

0 comments:

Post a Comment