ZAIDI YA MITI ELFU SITA YA MBAO YAPANDWA KATA YA IKUNA NJOMBE
Zaidi ya miti ya mbao aina ya paina elfu sita mia tisa imepandwa katika kampeni ya upandaji wa miti katika kata ya Ikuna huku zaidi ya miti ya matunda elfu moja nayo imepandwa na wananchi wa vijiji vya ikuna kwa kushirikiana na viongozi wao ikiwemo ya serikali na ya taasisi binafsi.
Zoezi hilo limefanyika jana kwa vijiji vyote vya kata ya Ikuna kwa wananchi wa vijiji vinne kushiriki upandaji huo ambapo kijiji kimoja cha Mahalule hakikushiriki kutokana na sababu za kuhamishwa kwa afisa mtendaji wa kijiji hicho jambo ambalo limepelekea kulegalega kwa uhamasishaji juu ya upandaji wa miti katika maeneo ya vijiji vyao.
Akisoma taarifa fupi ya upandaji wa miti ya matunda mmoja wa wananchi wa kijiji cha Matiganjora bwana Aidan Muhema amesema shamba la matunda ya mtu binafsi limepandwa ekari saba nukta tano miti mia tisa 87 yenye thamani ya
shilingi milini tano laki saba na tisini na tatu elfu kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwakajana na mwaka huu 2014.
Afisa mtendaji wa kata ya Ikuna Jobu Fute amesema kuwa kwa upande wa miti ya matunda ya serikali jumla ya miti ya matunda aina ya parachichi thelathini imepandwa leo na wananchi wa kijiji cha Ikuna huku miti ya mbao kwa kijiji hicho kikipanda zaidi ya elfu tatu mia saba iliyopandwa katika ofisi ya kata ya shule ya msingi Ikuna.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti diwani wa kata ya Ikuna Valentino Hongori na Julius Salingwa wamepongeza kwa hatua kubwa iliyofanyika na wananchi wa vijiji vya kata hiyo na kwamba kata na wananchi wa vijiji vingine wanatakiwa kuiga mfano huo kwa manufaa ya serikali na wananchi ili kupunguza wimbi la umasikini kwa baadhi ya wananchi.
Awali wakizungumza wananchi wa kijiji cha Matiganjora wameshukuru kwa ushirikiano mkubwa unaofanywa na viongozi wa serikali kwa kuwahamasisha kupanda miti hiyo kwa manufaa yao huku wakiiomba serikali kusimamia sera ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji kwa kuzitembelea taasisi mbalimbali kuhakikisha zinaondoa miti isiyo rafiki kwa vyanzo vya maji pamoja na wananchi kutekeleza agizo hilo.
kwa Hisani ya Michael Ngilangwa blog
0 comments:
Post a Comment