tg

Friday, January 17, 2014

HATIMAYE CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA NJOMBE KIMETANGAZA RASMI KUFANYA KAZI NA JESHI LA POLISI


kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Akizungumza na Uongozi wa NPC Juu ya Mgogoro Uliokuwepo Baina Ya Chama Hicho na Jeshi la Polisi.


Na  Mwandishi Wetu Toka NPC

Chama cha Waandishi wa Habari Mkaoni Njombe NPC Jana Kimetangaza Rasmi Kufanyakazi na Jeshi la Polisi Mkoani Njombe, Ikiwa ni Takribani Mwezi Mmoja Umepita Tangu Chama Hicho Kutofanyakazi na Jeshi Hilo, Kufuataia Mwandishwa wa Habari Michael Ngilangwa Kushmbuliwa na Baadhi ya Washabiki wa Timu ya Polisi na Askari Pamoja na  Kunyang'anywa Vifaa Vyake Vya Kazi

Akitangaza Kufanyakazi na Jeshi Hilo Katibu wa NPC Hamis Kasapa Amesema Chama Kimetoa Tamko la Kufanyakazi na Jeshi Hilo Baada ya Kuzungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Kuahidi Askari Waliohusika Kumshambulia Mwandishi na Kumnyang'anya Vifaa Vyake Vya Kazi Hatua za Kisheria Zina chukuliwa Dhidi Yao



AKizungumzia Tukio Hilo Ofisini Kwake SACP Ngonyani Amesema Jeshi la Polisi Mkoani NjombeLinalani Kitendo Hicho na Kusema Kuwa Tayari Askari Waliotajwa Kuhusika Kumshambulia Mwandishi Huyo Wanashikiliwa Kwa Mahojiano Zaidi, Kama Anavyoeleza

Hata Hivyo SACP Ngonyani Ameahidi Kutoa Ushirikiano Katika Kuhakikisha Vifaa Vya Mwandishi Huyo Vinapatikana na Hivyo Kuwaomba Wanahabari Kuendelea Kushirikiana na Jeshi Hilo.

Tukio la Kushambuliwa Kwa Mwandishi Huyo Lilitokea Novemba 24 Mwaka Jana Akiwa Anatekeleza Majukumu Yake Katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe Wakati wa Mchezo wa Mpira wa Miguu Baina ya Timu za Polisi FC na Njombe Mji FC .

0 comments:

Post a Comment