tg

Friday, January 17, 2014

WILAYA YA NJOMBE YAPIGA MARUFUKU KULIMA KWENYE VYANZO VYA MAJI

Na Gabriel  Kilamlya Njombe
Serikali Wilayani Njombe Imeagiza Kusitishwa Kwa Shughuli za Kilimo Kwenye Vyanzo Vya Maji Kutokana na Uharibifu Mkubwa Unaofanywa na Shughuli za Binadamu Katika Mazingira

Agizo Hilo Limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Shaibu Masasi Kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Wakatika Wa Uzinduzi wa Siku ya Upandaji Miti Katika Wilaya ya Njombe.

Akizungumza Mara Baada ya Uzinduzi Huo Makamu Mwenyekiti Huyo Bwana Masasi Amesema Kuwa Kitendo Cha Wananchi Kuendelea Kulima Kwenye Vyanzo Vya Maji Ilihali Wanaendelea Kupanda Miti,Kwani ni  Sawa na Kupoteza Nguvu kazi na Kuharibu Vyanzo Vya Maji.

Hatua Hiyo Imekuja Kufuatia Kuwepo Kwa Baadhi ya Wananchi Wanaoendeleza Shughuli za Kilimo Kwenye Chanzo cha Maji Cha Lupembe Barazani Ambako Limefanyika Zoezi la Uzinduzi wa Siku ya Upandaji Miti Katika Wilaya ya Njombe.

Awali Akisoma Risala Ya Siku ya Upandaji Miti  Iliyofanyika Januari 15 Mwaka Huu Katika Wilaya Ya Njombe Kwa Kuziunganisha Halmashauri za Mji Njombe na Halmashauri ya Wilaya,Afisa Kilimo na Umwagiliaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bi.Elitha Mligo Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo Amesema Kuwa Pamoja na Uharibifu wa Vyanzo Vya Maji Unaoendelea Kufanyika Lakini Halmashauri Imeendelea Kuhamasisha Suala la Uhifadhi na Upandaji Miti Hadi Kuvuka Lengo Walilojiwekea.

Bi.Mligo Amesema Kuwa Katika Kipindi cha Mwaka 2014 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ilipanga Kuotesha Miche 15,000,000 Ya Aina Mbalimbali Lakini Hadi Sasa Wamefanikiwa Kuotesha Miche  22,885,650 Inayotarajiwa Kupandwa Katika Kipindi Cha Mwaka 2013/2014,na Hapa Anaelezea.

Zoezi la Upandaji Miti  Hufanyika Januari Mosi Kila Mwaka na Hivyo Kila Halmashauri Ilipangiwa Kufanya Zoezi Hilo Kutegemeana na Hali ya Hewa Hivyo Wilaya ya Njombe  Imefanya Uzinduzi Huo Januari 15 Mwaka Huu Katika Kijiji Cha Lupembe na Tarafa ya Lupembe.

Kaulimbiu ya Siku ya Upandaji Miti Kwa Mwaka Huu Inasema"MITI NI MALI,PANDA MITI KWANZA NDIPO UKATE MTI"

0 comments:

Post a Comment