Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua
Mheshimiwa Pindi Chana kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu na Michezo ya
kuigiza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Uteuzi
huu unatokana na Mamlaka aliyopewa Waziri huyo chini ya kifungu cha
13(i) cha Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na.4. ya mwaka 1976.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo kwa Vyombo vya habari uteuzi wa
Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Bodi umeanza tarehe 3 Desemba 2013.
Aidha
Waziri huyo amewateua Wakili wa Kujitegemea Silvester Sengerema ,Dr.
Vicensia Shule kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Bishop Hiluka
kutoka Shirikisho la Filamu Tanzania kuwa wajumbe wa Bodi hiyo katika
kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Wajumbe
wengine ni Jacob Sarungi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,
Ntobi Fredrick kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, na Joyce Fissoo
ambaye ni Katibu wa Bodi ya Filamu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
0 comments:
Post a Comment