tg

Friday, January 24, 2014

MLINZI AUWAWA KINYAMA NA WATU WASIYOFAHAMIKA KATIKA MTAA WA RAMADHANI HUKU GODAUNI LA STACO AGRO CHEM IKIVAMIWA MKOANI NJOMBE








Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.


  Mkazi mmoja wa kijiji cha Ulembwe wilayani wanging'ombe Stivin Kiswaga ameuwawa na watu wasiyo fahamika usiku wa kuamkia jana  akiwa katika lindo kwenye duka la bwana Fred Mbilinyi mkazi wa mtaa wa Ramadhani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa mtaa wa Ramadhani wamesema wamesikitishwa na kitendo cha kutokea kwa tukio hilo huku wakiiomba serikali kuanzisha mpango wa ulinzi shirikishi ili kudhibiti matukio ya ujambazi na mauaji yasijitokeze tena.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tisa alfajiri ambapo watu wasiyofahamika wamefika katika duka la bwana Mbilinyi na kumvamia mlinzi huyo na kisha kumtupa kwenye nyumba za jirani umbali wa takribani mita mia moja toka tukio lilipotokea.

Mwenyekiti wa mtaa wa Ramadhani Bashiry Sanga amesema wananchi wanatakiwa kuonesha ushirikiano kwa kuwahi kufika eneo la tukio pindi mwananchi anapopiga kelele za kuvamiwa na majambazi ili kumunusuru uhai wake kuliko kuendelea kujificha jambo ambalo linapelekea kushindwa kuokoa maisha na mali za baadhi ya wahanga wa tukio husika.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu huyo alikuwa mlinzi wa mfanyabiashara wa mtaa wa Ramadhani bwana Fred Mbilinyi ambapo amepigwa na kitu kizito kichwani kisha kutolewa sikio lake moja na kutupwa umbali wa mita mia moja na kwamba hakuna watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo na uchunguzi bado unaendelea.

Wakati huohuo Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limethibitisha kutokea kwa matukio mawili
ya unyang'anyi na wizi wa pikipiki aina ya bajaji mkoani Njombe ambapo
pamoja na mambo mengine jeshi hilo bado linaendelea na jitihada za
kuwatafuta waharifu waliohusika na matukio hayo.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe
SACP Fulgence Ngonyan amesema kuwa tukio la kwanza limetokea january 22
mwaka huu katika godauni la Staco mtaa wa mwembetogwa ambapo watu
wasiyofahamika walivamia godauni la Staco Agro Chem mali ya Tyson Shivilal
na kumjeruhi mtunza stoo Juma Kahelo mkazi wa mtaa wa kivavi katika halmashauri ya mji wa  makambako.

Aidha kamanda Ngonyani amesema kuwa katika tukio hilo wezi hao
walifanikiwa kupora kiasi cha shilingi milioni kumi na mbili na laki tano
mali ya kampuni hiyo pamoja na simu ya mkononi aina ya nokia Asha yenye
thamani ya shilingi laki moja na tisini Mali ya Lydia Mkurasa ambae
alikuwa ni meneja wa kampuni hiyo.

Katika tukio lingine kamanda Ngonyani amesema kuwa watu wasiyofahamika
wameiba pikipiki aina ya bajaji yenye thamani ya shilingi milioni sita
yenye namba za usajili T 559 CJU mali ya Gastor Mbavile mkazi wa mtaa wa
national housing iliyokuwa imepaki mbele ya duka lake mkabala na barabara
ya Njombe-Songea eneo la mlimani park mjini Njombe.

Amesema kuwa tukio hilo limetokea january 22 mwaka huu majira ya saa saba
na dakika hamsini ya  mchana katika mtaa wa Mliman motel kata ya Njombe
mjini na kwamba jeshi la polisi linaendelea kuwasaka waharifu hao huku
likiwataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi matukio ya uharifu
yanapojitokeza ili kuwahi eneo la tukio na kuwabaini waharifu hao.

Na Michael Ngilangwa, Njombe

0 comments:

Post a Comment