Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruan Akitangaza Wanafunzi Watakaojiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2014
Sekretarieti ya Elimu Mkoa wa Njombe Wakati wa Kutangaza Nafasi za Kujiunga na Kidato cha Kwanza Hapo Januari Mwaka 2014.
Matokeo Hayo Yametangazwa Disemba 28 Mwaka Huu Katika Ukumbi huo Mjini Makambako
Baadhi ya
Wadau wa Elimu Wakiwa Kwenye Kikao Hicho Jana Mjini Makambako Kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akifuatiwa na Kaimu Katibu
Tawala Wilaya ya Njombe.
Habari kamili........................................................
Halmashauri
ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe Imeonekana Kuongoza Katika Matokeo ya
Mtihani wa Darasa la Saba Kimkoa Ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji
Njombe Kwa Mwaka 2013
Licha ya Matokeo hayo Yaliyopelekea Mkoa
wa Njombe Kushika nafasi ya Tano Kitaifa Kati ya Mikoa 25 ya Tanzania
Bara lakini Shule ya Msingi Kanani Iliyopo Wilayani Wanging'ombe
Imefanikiwa Kutoa Mwanafunzi bora wa kwanza Kimkoa Anayejulikana kwa
Jina la Neema Wihallah.
Akitangaza Matokeo Hayo Wakati wa
Kuwapanga Wanafunzi hao Afisa Elimu Mkoa wa Njombe Bwana Said Nyasilo
Kwa Mwaka 2013 Jumla ya Watahiniwa 18752 Wakiwemo Wavulana 8698 na
Wasichana 10,967 sawa na Asilimia 59.0% Isipokuwa kwa Halmashauri ya
Mji wa Makambako.
Aidha Jumla ya Wanafunzi 379 Wakiwemo Wavulana
155 na Wasichana 224 Wamekosa nafasi katika shule za Sekondari Kutokana
na Upungufu wa Vyumba vya Madarasa na Uchache wa Shule Hizo.
Hata
Hivyo Mwaka 2013 Jumla ya Wanafunzi 275 Wakiwemo Wavulana 170 na
Wasichana 105 sawa na Asilimia 1.4% hawakufanya Mtihani Huo
Ikilinganishwa na Wanafunzi 571 sawa na Asilimia 2.9% ya Mwaka 2012.
Kutokana
na Hali Hiyo Mkoa wa Njombe Umewatangaza Jumla ya Wanafunzi 10984
Wakiwemo Wavulana 4884 na Wasichana 5800 Sawa na Asilimia 97% ya
Wanafunzi Waliopata Alama 100 hadi 250 Wamechaguliwa Kujiunga na Masomo
ya Kidato cha Kwanza Mwaka 2014.
Na Gabriel Kilamlya, Makambako.
0 comments:
Post a Comment