Muonekano wa Basi la Ukinga Express likiwa kwenye eneo la ajali.
Abiria
waliokuwa wakisafiri kwa basi la Ukinga Express kutoka Njombe kwenda
Makete mkoani Njombe, wamenusurika kifo baada ya basi hilo walilokuwa
wakisafiria kuigonga fuso kwa nyuma iliyokuwa imepata hitilafu na
kuegeshwa barabarani
Ajali
hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo linalohofiwa na wengi la
Lwamadovela kata ya Tandala wilayani Makete, baada ya dereva wa basi
hilo kuigonga kwa nyuma fuso hiyo ambayo ilipata hitilafu kwenye eneo
lenye kona
Wakizungumza
na mwandishi wa eddy blog aliyefika eneo la tukio na kushuhudia ajali
hiyo, mashuhuda hao bila kutaja majina yao wamesema chanzo cha ajali
hiyo ni dereva wa basi hilo kushindwa kulimudu gari lake licha ya kuwepo
na kona kali, lakini pia mwenye fuso alishindwa kuweka ishara za
kutosha kuonesha kama gari lake limepata hitilafu barabarani
"Unajua
braza(akimaanisha kaka) dereva huyu wa hili basi alikuwa mwendo na ndio
maana ghafla alipoanza kukunja kona akakutana na hii fuso mbovu, kwa
kuwa alikuwa na mwendo kasi ilikuwa ngumu kushika breki ingawa
alijitahidi kama unavyoona lakini ilishindikana, ndipo akaigonga hii
fuso kwa nyuma" alisema shuhuda huyo
wamesema
kutokana na ajali hiyo, baadhi ya abiria walipata majeraha hasa
waliokuwa wamekaa viti vya mbele, ingawa mashuhuda hao hawakujua mara
moja ni idadi ya abiria wangapi wameumia na hali zao zikoje
Hadi
mwandishi wetu ambaye alikuwa akipita eneo hilo kuendelea na safari na
kukutana na tukio hilo anaondoka eneo hilo, polisi walikuwa wakisubiriwa
kuja kupima na kufanya taratibu za kijeshi kuhusu ajali hiyo, hivyo
kuacha wananchi waliokuwepo eneo hilo wakiwasubiri
Ikumbukwe
kuwa eneo hilo lililotokea ajali hiyo halina mtandao wa simu, hivyo
aliyekuwa akitaka mawasiliano alikuwa akitembea umbali mrefu kutafuta
mtandao, hali inayodaiwa kuchelewesha kufikisha taarifa hizo kwa polisi
Makete mjini
Picha zote za tukio hilo zinakujia punde, endelea kusoma EDDY BLOG na www.edwinmoshi.com
KWA IDHINI YA AMINIA WEBSITE
0 comments:
Post a Comment