tg

Monday, December 16, 2013

MASHINE YA KUKAGUA DAWA ZA KULEVYA YANUNULIWA


Uongozi  wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) uliopo Dar es Salaam, umenunua mashine mpya ya kukagua dawa za kulevya. Akizungumza na RAI Jumatatu Dar es Salaam jana, Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Renatus Chaly, 

alisema wameamua kununua mashine hiyo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kutokana na usafirishaji haramu wa dawa za kulevya ambazo zimekuwa janga la Taifa.


 Alisema kutokana na matukio mengi kama hayo kujitokeza mara kwa mara, wameamua kujipanga upya na wameimarisha ulinzi sehemu zote katika viwanja hivyo. 

 “Tumeimarisha ulinzi sehemu zote katika uwanja huu, kwa sababu wafanyabiashara haramu wa dawa za kulevya wamekuwa wakipita kwa njia nyingi, ikiwa ni pamoja na wanawake kumeza au kuweka sehemu za siri dawa hizo na kuzisafirisha kwenda nje ya nchi.

 “Ulinzi katika kiwanja hiki umeimarika na tunaendelea kujipanga zaidi kuweza kutokomeza kabisa usafirishaji wa biashara hii haramu ya dawa za kulevya,” alisema Chaly.

 Aliwaomba Watanzania waepukane na biashara ya dawa za kulevya, kwa sababu yanairudisha nchi nyuma. Aliwataka wananchi kuonyesha ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapoona watu wanafanya biashara hiyo. 
 Chanzo-Rai 

0 comments:

Post a Comment