tg

Saturday, August 9, 2014

KAMANDA WA POLISI MKOA WA NJOMBE APATA AJALI, "BODY GUARD" WAKE AFARIKI DUNIA.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani.

Na James Festo, Njombe.

KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  pamoja na dereva wake Nuaka Seme  wamelazwa katika hispitari ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea  kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia  jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.

Akiongea na vyombo vya habari  huku akipatiwa matibabu katika hospitari ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP Yahaya  rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hanaruhusa Kamanda Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa nne za usiku katika barabara ya  Makambako hadi Njombe.

Aidha Jeshi la Polisi  limesema kuwa  katika ajali hiyo aliyefariki dunia ni George  Stephano  Matiko (24)

 H580 Pc George  Enzi za uhai wake.
Nuaka Sema aliyekuwa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili PT 2058  alisema kuwa kutokana  gari hilo la mizigo kukaa katikati ya barabara walishindwa kupishana kwa wakati na kuligonga kwa nyuma na baadae kukutana uso kwa uso na nguzo ya umeme iliyowasababishia ajali.

"ghafla niliona gari mbele likiwa limewasha taa zote za mbele (full light) likiwa upande wetu na nilivyoona hivyo niliwasha taa kuashiria hatari  na ndipo mwenye gari la mizigo alianza kukwepa kuelekea upande wake na wakati tukipishana mwishoni kwa kuwa lilikuwa refu tulienda tukakwanguana ndipo tulipoteza mwelekeo" alisema dereva huyo.

Aliongeza kuwa " mara baada ya kukwanguliwa tukilikwepa lori tukaigonga nguzo ya umeme na hapo hapo mwenzetu akafariki na tunashukuru sana wafanyakazi wa kampuni ya tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na lile lori hatukuweza kuchukua namba zake na liliendelea na safari".

Kwa upande wake  Afisa muuguzi wa hospitari hiyo  Bw. Denis Haule alisema kuwa majeruhi wawili  walipokelewa majira ya saa tano usiku na mwingine  alikuwa amekwisha fariki dunia na kubainisha kuwa hali ya majeruhi hao inaendelea vizuri na  Kamanda wa Polisi anaweza kuruhusiwa muda wowote.

"tumewapokea jana usiku  majeruhi  wawili na mmoja  akiwa amekwisha fariki dunia , hali yao kwa sasa inaendelea vizuri  na kamanda anaweza kuruhusiwa wakati wowote....lakini dereva wake anatakiwa kuendelea kupewa matibabu kutokana na maumivu mbalimbali katika mwili wake.

.............................MWISHO...........................

0 comments:

Post a Comment