tg

Friday, January 24, 2014

WATATU KIZIMBANI KWA WIZI WA RECEIVER YA Tshs.MILIONI 16 MALI YA SHULE YA SEKONDARI KIFANYA NJOMBE


Wakazi Watatu wa Kijiji cha Kifanya Wilayani Njombe Maurus Chengula, Victorn Yordan  Maarufu Kwa Jina la Mayemba na Raymond Chengula Wamefikishwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe na Kusomewa Shtaka la Wizi wa GPS Receiver Yenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 16 Mali ya Shule ya Sekondari Kifanya.

Akisoma Hati ya Mashtaka Mbele ya Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo, Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali Yahaya Misango Ameiambi Mahakama Kuwa Washtakiwa Hao Ambao ni Walinzi wa Shule Hiyo Walitenda Kosa Hilo Januari Sita Mwaka Huu.

Hata Hivyo Washtakaiwa Walipohojiwa Kuhusika na Kosa Hilo Wamekana , Huku Mwendesha Mashtaka Wakili Huyo wa Serikali Akiiambia Mahakama Kuwa Upelele Juu
ya
Wizi Huo Bado Unaendelea .

Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Februari Nne Mwaka  Huu Kesi Hiyo Itakaposikilizwa Mara Baada ya Upelelezi Kukamilika Huku Akisema Dhamana Kwa Washtakiwa Iko Wazi.

0 comments:

Post a Comment