Shule ya Msingi Ruhuji B Iliyopo Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Imeshindwa Kuanza Muhula wa Masomo Kwa Mwaka Huu Kama Ilivyokuwa Imetarajiwa Kutokana na Shule Hiyo Kutokamilika .
Akiongea na Uplands Redio Afisa Elimu Shule ya Msingi Halmashauri ya Mji wa Njombe Zegeli Shengeli Amesema Shule Hiyo Ambayo ni Mpya Haiwezi Kuanza Muhula wa Masomo Kwa Sasa Kutokana na Mapungufu Yaliyopo Katika Shule Hiyo na Kuongeza Kuwa Ili Shule Hiyo Ifunguliwe Kunahitajika Vyumba Vitatu na Ofisi za Walimu.
Afisa Elimu Huyo Amesema Licha ya Jitihada za Wananchi na Wadau wa Elimu Kukamilisha Ujenzi wa Vyumba Vinne Kwa Ajili ya Madarasa Pamoja na Vyoo Lakini Wananchi Hao Wanatakiwa Kuongeza Vyumba Viwili na ofisi za
Walimu Ili Kukidhi Mahitaji Shuleni Hapo.
Wananchini Mjini Njombe Kwa Kushirikiana na Wafanyabiashara Walianzisha Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Ruhuji B Kwa Lengo la Kutaka Kupunguza Msongamano wa Wanafunzi Uliopo Katika Shule ya Msingi Ruhuji.
Shule Mpya ya Msingi Ruhuji B Ilitarajiwa Kuanza Kupokea Wanafunzi wa Muhula wa Masomo Mwaka Huu Lakini Hadi Sasa Imeshindwa Kufanya Hivyo.
Kwa Kushindwa Kufunguliwa Kwa Shule Hiyo Katika Kipindi cha Mwaka Huu Kunawafanya Wazazi na Wananchi Kufanya Kazi ya Ziada ya Kuanza Kuchangia Upya Michango Mingine
0 comments:
Post a Comment