Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mkuu wa Mkao wa Njombe Keptein Mstaafu Asseri Msangi LEO Anatarajia Kuwa Mgeni Rasmi Katika Siku ya Uhamasishaji wa Kilimo cha Zao la Viazi Mviringo Litakalofanyika Kwa Siku Mbili Mkoani Njombe na Kuwakutanisha Wataalamu na Wakulima wa Zao Hilo.
Kwa Mujibu wa Taarifa Iliyotolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kilimo Njombe NADO John Wihallah Imesema Katika Siku Hizo Mbili Mada Mbalimbali Zitatolewa Pamoja na Majadiliano Juu ya Kuboresha Kilimo cha Viazi Mviringo Katika Maeneo Yao na Kukifanya Kiwe na Tija.
Aidha Mkurugenzi Huyo wa NADO Amesema Zao la Viazi Mviringo Limeonekana Kutokuwa na Tija Kutokana na Baadhi ya Wakulima Kutotumia Mbegu Bora za Viazi na Kufuata Kanuni za Kilimo cha Kisasa na Kwamba Kupitia Uhamasishaji Huo Utawasaidia Wakulima Kuboresha Shughuli Zao za Kilimo.
Ameongeza Kuwa Washiriki wa Uhamasishaji Huo Wapata Fursa ya Kutembelea Kutembelea Katika Maeneo Mbalimbali ya Wakulima Hao na Kujifunza Shughuli Zinazofanywa na Wakulima Hao Pamoja na Maonesho .
Uhamasishaji Huo wa Kilimo cha Viazi Mviringo Utahudhuriwa na Wadau Kutoka Jijini Mbeya , Halmashauri za Wilaya na Mji wa Njombe , Wanging'ombe na Wageni Kutoka Nje ya Nchi, Chini ya Ufadhili wa SAGCOT.
0 comments:
Post a Comment