Baadhi ya Madiwani Wakiwa Kwenye Kikao cha Baraza leo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Dustan Shimbo Akiwasilisha Kanuni Mpya za Halmashauri Hiyo Leo Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.
Wataalamu Mbalimbali Wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Na Gabrie Kilamlya Njombe
Wakati Serikali Ikianza Kuboresha Kanuni za Kudumu Za Halmashauri Mbalimbali Hapa Nchini ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Imeagiza Kuwepo Kwa Kipindi cha Maswali Ya Papo Kwa Papo Kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya au Mkurugenzi Katika Kikao Cha Baraza la Madiwani.
Kanuni Hizo Tayari Zimeshafikishwa Katika Kila Halmashauri Nchini na Kwamba Zinatakiwa Kuanza Kutumika Mapema Iwezekanavyo Huku Wajumbe wa Baraza la Madiwani Wakitakiwa Kupata Semina Juu ya Uendeshaji wa Halmashauri Kwa Kutumia Kanuni Hizo.
Akizungumza Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Leo Mwanasheria wa Halmashauri Hiyo Bwana Dustan Shimbo Amesema Kuwa Kanuni Hizo Zinapaswa Kuanza Kutumika Katika Kikao Cha Baraza la
Madiwani Kijacho Hivyo Madiwani Hao Wanapaswa Kupata Semini Mapema Iwezekanavyo.
Mwanasheria Huyo Pia Amesema Kwa Mujibu wa Kanuni Hizo Zimebainisha Mambo Mbalimbali Ikiwemo Utaratibu wa Kumchagua na Kumuondoa Mwenyekiti wa Halmashauri Madarakani Pamoja na Utaratibu wa Kuwepo Kwa Maswali ya Papo Kwa Papo.
Akizungumzia Kuhusu Utaratibu wa Uulizaji Maswali Hayo ya Papo Kwa Papo Mwanasheria Huyo Amesema Mjumbe Yeyote Anapaswa Kuoredhesha Jina Lake Kwa
Mwenyekiti Au Mkurugenzi Atakayeulizwa Maswali Hayo Katika Kipindi cha Saa 24
Kabla ya Kuanza Kwa Mkutano wa Baraza la Madiwani.
Bwana Shimbo Amesema Kanuni Hizo Zimeboreshwa Kwa Hatua za Awali Kwani
Zitafanya Kazi Kubwa ya Kuwaweka Sawa Madiwani Hao Kwenye Vikao Vyao Ikiwa
ni Pamoja na Kuboresha Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali Katika Halmashauri Hiyo .
Katika Hatua Nyingine Kanuni Hizo Zinawataka Madiwani Hao Kuwasilisha Matatizo
Mbalimbali ya Kata Zao Kwenye Kikao Cha Kwanza Cha Baraza Hususani Katika
Masuala ya Majanga Mbalimbali Kwenye Eneo la Kata Husika,Masuala ya
Kielimu,Afya,Maendeleo Ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Vitakavyobainisha Uwepo wa
Wataalamu,Zana za Kisasa na Pembejeo za Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Sanjari na Hayo Lakini Pia Mambo Mengine Yanayopaswa Kuzungumzwa Kutoka
Kwenye Kata Hizo ni Pamoja na Uimarishaji wa Dhana ya Uzalendo na Utaifa Kwa
Kuhamasisha Vijana Kuanzisha Kujiunga na Vikundi Vya Vijana Wagani Kazi na
Mafunzo ya Jeshi la Mgambo,Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii.
0 comments:
Post a Comment