Gari la mkuu wa mkoa wa Njombe likiwa limekwama kwenye tope kijiji cha utweve makete.
Wadau wakisukuma gari hilo, na huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Utweve akijitahidi kusukuma.
Hali tete hapa, gari hilo likiwa limenasa mtaroni
wadau wakijitahidi kuvuta gari hilo
jitihada zikiendelea.
Gari
la mkuu wa mkoa wa Njombe, kapteni mstaafu Aseri Msangi limekwama kwa
zaidi ya saa kadhaa katika kijiji cha Utweve wilayani Makete wakati
akiwa ziarani kukagua maendeleo ya sekondari ya wasichana makete
inayojengwa kijijini hapo
Adha
hiyo ilimkumba mkuu wa mkoa baada ya mvua kubwa kunyesha wakati
akifanya mkutano na wananchi shuleni hapo mara baada ya kuikagua shule
hiyo na kuridhishwa na jinsi ilivyojengwa
Mtandao
huu wa eddy blog umeshuhudia magari mengine yaliyokuwa yametangulia
gari la mkuu wa mkoa yakipita eneo hilo lililokuwa na utelezi mwingi
huku gari hilo la mkuu wa mkoa likikwama kutokana na utelezi huo
Jitihada
za kulinasua gari hilo zilifanywa na msafara mzima ulioambatana na mkuu
wa mkoa pamoja na wananchi wa kijiji hicho ambapo zoezi hilo lilichukua
zaidi ya saa moja kutokana na mvua kuzidi kunyesha zaidi
Jitihada
hizo zilizaa matunda na hatimaye gari hilo lilinasuliwa na mkuu wa mkoa
kuendelea na safari yake, na hakuna madhara yoyote yaliyotokea
0 comments:
Post a Comment