tg

Saturday, February 15, 2014

HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE IMEPOKEA TSH BILIONI 2.1 KWA AJILI YA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

 Wa Kwanza Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Shaib Masasi,Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri Bwana Valence Kabelege na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Paulo Malala.
 Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Wakiwa Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Kujibia Hoja Mbalimbali.


 Baadhi ya Madiwani Wakipitia Makablasha yao Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani
 Ofisa Kilimo na Umwagiliaji Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bi.Elitha Mligo Akitolea Ufafanuzi Juu ya Kusimama kwa Kiwanda cha Matunda Madeke.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Dustan Shimbo Akizungumza Jambo Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani

 Na Gabriel  Kilamlya Njombe

Katika Kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 Halmashauri ya wilaya ya Njombe imepokea jumla ya shilingi bilioni 2,105,690,718.50 hadi kufikia mwezi disemba mwaka jana ambazo ni sawa na asilimia 40 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Fedha hizo ni kati ya shilingi bilioni 5,259,737,669.65 zilizoidhinishwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/2014 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo katika halmashauri ya wilaya ya Njombe.

Akiwasilisha taarifa ya utekeleza wa miradi ya maendeleo ya robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2013/2014,kaimu ofisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya

Njombe Bi.Waza Benjamin alisema kuwa kati ya fedha hizo zilizopokelewa tayari baadhi zimeanza kutekeleza miradi hiyo licha ya kuwa bado kuna changamoto kubwa ya kuchelewa kwa fedha hizo.

Aidha Bi.Benjamin alieleza kuwa kati ya fedha hizo zilizopokewa jumla ya shilingi bilioni 1,191,240,966.91 tayari zimeshatumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya halmashauri hiyo ambazo ni sawa na asilimia 57 ya fedha zilizopokelewa

Katika hatua nyingine baadhi ya miradi inayoendelea kutekelezwa kutokana na fedha Zilizofika ni Pamoja na Sekta ya Ushirika,Maendeleo ya Jamii,Ujenzi na Miundombinu Mbalimbali .

0 comments:

Post a Comment