Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga
Na Gabriel Kilamlya
Akizungumza na Uplands Fm Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Amesema Kuwa Kinachofuata Kwa Sasa ni Kila Mmoja Ndani ya Kata Ya Njombe Mjini Kuhakikisha Anaendelea Kufanya Kazi Hususani Kwa
Kuendeleza Kile Alicho Kiache Aliyekuwa Diwani wa Kata Hiyo Ndugu Lupyana Fute Enzi za Uhai Wake.
Bwana Mwanzinga Pia Amesema Kwa Wale Watakao Onekana Wanaendeleza Siasa Ilihali Uchaguzi Umeisha Ni
Wazi Kwamba Siasa Hawazijui Hivyo Hawanabudi Kuachana Nazo.
Aidha Amewataka Wananchi Hao Pamoja na Wenyeviti wa Mitaa Ambao Wanatokana na Chama Tawala cha Mapinduzi Kuonesha Ushirikiano Mkubwa Kwa Diwani Wao Ambaye Ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata Hiyo Anayetokana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Pamoja na Mambo Mengine Bwana Mwanzinga Amewataka Wananchi Kuepukana na Utofauti wa Itikadi za Kisiasa Kwani Kwa Sasa Kinachotakiwa ni Kuangalia Namna Ya Kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010/2015.
Agrey Mtambo ni Diwani Mteule wa Kata ya Njombe Mjini Kupitia Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ambapo Muda Wowote Mara Baada ya Kuapishwa Rasmi Ataanza Kufanya Kazi na Wananchi wa Kata Ya Njombe Mjini Katika Kusogeza Mbele Gurudumu la Maendeleo.
Muda Wowote Kuanzia Sasa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Atatoa Taarifa Ya Kuapishwa Kwa Diwani Huyo Ambaye Alichaguliwa Februari Tisa Mwaka Huu Katika Uchaguzi Mdogo wa Diwani Kata Ya Njombe Mjini Kati ya Kata 27 Zilizofanya Uchaguzi Huo Nchini Kote.
0 comments:
Post a Comment