huyu ndiye bw Evagrey Keiya Anayeshitakiwa kwa kosa la kufanya manunuzi hewa pamoja na mhasibu wake enzi akikaimu nafasi ya DAS. picha na maktaba
Na James Festo,Njombe
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi hapo jana ametolea ushahidi mbele ya mahakama ya Wilaya ya Njombe dhidi ya kesi ya manunuzi hewa wa magurudumu matano na betri mbili za gari vyoti vikiwa na thamani ya shilingi milioni 14 inayomkabili aliyekuwa kaimu katibu tawala wa wilaya hiyo ya wanging'ombe bw evegray keiya.
Akitoa ushahidi wake mahakamani hapo , mkuu huyo wa Wilaya ya Wanging'ombe ambaye ni shahidi namba moja ameiambia mahakama kuwa ofisi yake pamoja na aliyekuwa akikaimu ofisi ya katibu tawala Wilaya ya Wanging'ombe waliagiziwa magurudumu tano aina ya gunrub kwa ajili ya gari yake lakini hakuwahi kuyaona magurudumu hayo katika ofisi yake .
kwa kipindi kile yanaletwa magurudumu hayo nilikuwa natumia gari niliyopewa na Halmashauri ya Wilaya Njombe kwa kipindi hicho sikuwa na umuhimu wa magurudumu hayo lakini baada ya miezi mitatu baadae nilipotaka kubadili magurudumu sikuyaona........alisema Bi Kilasi
Akitoa ushahidio mahakamani hapo shahidi namba mbili ambaye ni afisa manunuzi wa Mkoa wa Njombe Gaitan Malio Lugenge aliiambai mahakama kuwa alipokea taarifa ya ununuzi wa magurudumu matano na betri mbili aina ya n70 na kusema kuwa betri moja liliwekwa kwenye gari lenye namba za usajili stj 6821 ya katibu tawala Mkoa wa Njombe .
Akiendelae kutoa ushahidi mahakamani hapo shahidi namba mbili Gaitan Malio Lugenge
Ameieleza mahakama kuwa magurudumu waliyoyapokea yalikuwa tofauti na yale yaliyoagizwa yanunuliwe kwani magurudumu waliyoyapokea yalikuwa ni bridgestoni badala ya gunrub.
Kwa upande wao washtakaiwa wakitetewa wakili wao hawakutakiwa kujibu chochote
Mara baada kusikiliza utetezi wa upande wa mashtaka hakimu wa mahakama hiyo John kapokolo ameahirisha kesi hiyo hadi machi tano mwaka huu itakapo sikilizwa tena mahakamani hapo na washitakiwa wameachiwa kwa dhamana.
Na katika kesi nyingine Anna Wiketye (33) mkazi wa mtaa wa bomani kwenye halmashauri ya mji njombe ambaye pia ni afisa tawala wa Wilaya Njombe amefikishwa mahakamani hapo ili kujibu shtaka linalo mkabili ambapo inadaiwakuwa alitoa ushahidi wa uongo kinyume na kifungu cha sheria namba 102 sura ya kwanza na kifungu namba 104 sura ya 16 cha sheria zas kanuni za makosa ya adhabu katika kesi inayomkabili aliyekuwa katibu tawala wa halmashauri ya wilaya ya njombe.
Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali bw Riziki Matitu alisema kuwa mnamo novemba 18 mwakajana mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo ili kutolea ushahidi wa kesi ya .Bori Salonge Ally, Evegray Keiya na Ibrahim Konga na kutoa ushahidi wa uongo ulioufanya upande wa mashitaka kumuondoa katika orodha ya mashahidi kwenye kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kusababisha hasara ya shilingi milioni mbili za Halmashauri hiyo.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitoa ushahidi ambao unakinzana na ushahidi aliowahi kutoa alipokuwa akihojiwa na taasisi ya kupambana na rushwa ushahidi unaosema kuwa alitoa kibali cha mafuta ya mafuta ya gari binafsi kwa matumizi ya ofisi badala yake mafuta hayo yalitumiwa kwa matumizi binafsi.
Kwa upande wake mshitakiwa akijibu mashtaka yanayomkabili amekubali kutoa maelezo hao kwa maofisa wa takukuru na kusema kuwa ushahidi huo aliutoa kutokana na mazingira aliyokuwa nayo wakati akihojiwa katika ofisi hizo na haukuwa hiari yake.
Katika kuhakikisha haki inapatikana mahakamani upande wa jamhuli umenuia kuwaita mashahidi watatu ambao ni Rehema Mpagama,Roda Lupondo na Lukas Sweve huku vielelezo vikiwa ni hati ya maelezo kutoka takukuru.
Hata hivyo hakimu wa mahakama hiyo ameiahirisha kesi hiyo hadi tarehe tano mwezi wa tatu mwaka huu na mshitakiwa yuko nje kwa dhamana.
0 comments:
Post a Comment