tg

Thursday, January 30, 2014

HALI YA LISHE BORA WILAYANI MAKETE SI YA KURIDHISHA


 Afisa afya wilaya ya Makete Bw. Abraham Sanga(kulia) akizungumza kuhusu hali ya lishe katika studio za Kitulo Fm, kushoto ni mtangazaji wa kipindi Ergon Sanga.
======
Imeelezwa kuwa wilaya ya Makete mkoani Njombe ni miongoni mwa wilaya zenye matatizo ya lishe ambapo kwa mujibu wa utafiti imeonesha kuwa asilimia 60 ya watoto wilayani humo wamedumaa

Kauli hiyo imesemwa na Afisa lishe wilaya ya Makete Bw. Abraham Sanga wakati akizungumzia hali ya lishe katika wilaya ya Makete katika kipindi cha maisha ni afya kinachorusha na redio ya jamii Kitulo Fm iliyopo wilayani humo

Amesema utafiti huo ulifanywa kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Makete januari 2013 kwa kushirikiana na taasisi ya chakula na lishe (TFDA), na UNICEF ambapo imegundulika hali ya lishe wilaya ya Maketi si ya kuridhisha

Bw. Sanga amesema sababu ya watoto wengi kudumaa ni kuwa huanzia tangu tumboni kutokana na sababu ya ukosefu wa chakula bora muda mrefu hasa kwa wajawazito, ambapo amesisitiza ni vyema kwa wazazi kuhakikisha chakula bora kinapatikana kwa familia ili kuepukana na matatizo hayo

Pamoja na hali ya udumavu pia Bw. Sanga amezungumzia suala la ukondefu pamoja na umuhimu wa vitamini A mwilini kwa kuwa vitamini hiyo ni muhimu na inatumika kusaidia vitu vingi mwilini ikiwemo hali ya kuona vizuri hasa usiku, taifa kuwa na watoto wenye uwezo mzuri kiakili n.k
Miongoni mwa vyakula vinavyosababisha mtu kuwa na vitamini A kwa wingi ni mboga za majani kama mchicha, sukumawiki, tembele, majani ya maboga na pia ziwe za kijani kibichi na zisipikwe zikaiva sana 
 
credit EDDY BLOG 

0 comments:

Post a Comment