tg

Thursday, January 3, 2013

BUNGE FILIKUNJOMBE AWALIPUA WATUMISHI IDARA YA MAJI LUDEWA MBELE YA WANANCHI



MBUNGE  wa  jimbo la  Ludewa  mkoani Njombe Deo Filikunjombe (pichani)awalipua   watumishi wa idara ya maji katika Halmashauri ya  wilaya  ya Ludewa akidai  wanachelewesha mradi  wa maji  hivyo wanataka  kumchonganisha na  wapiga  kura  wake  wa  kijiji cha Maholong'wa kata ya Ludende ili akose  kura  mwaka 2015.
Akizungumza jana kwa jazba katika mkutano  wa hadhara  uliofanyika kijijini hapo  mbunge Filikunjombe ambae alilazimika  kumsimamisha mwakilishi  wa mhandisi wa maji  wilaya ya Ludewa Teudelin Mfute aliyemwakilisha mhandisi wa maji  wilaya ya Ludewa vijijini  ,ili aeleze  sababu ya  kuendelea  kuchelewesha mradi huo  wakati tayari  serikali imetoa  fedha kwa ajili ya kuanza mradi huo.
"Nataka  unieleze mhandisi  wa maji madunda kuna maji hakuna maji ....sasa kama Madunga unasema hakuna maji Maholong'wa  watapataje maji ...sasa watendaji wa Halmashauri mliopo hapa  naomba hi mtaniwia radhi kuwa idara ya maji Ludewa  kuna shida ila nawahakikishia kuwa  tutakaa tutalimaliza"
Alisema  haiwezekani  wananchi  wanatabika na kulia  juu ya ukosefu wa maji huku  watendaji  wa serikali wakiendelea  kukaa maofisini huku  wakilipwa pesa  bila  kufanya kazi .
Filikunjombe  alisema lazima atahakikisha  kila mtumishi  wa umma katika wilaya  hiyo ya Ludewa anatimiza  wajibu wake  kwa  kuwajibika kwa  wananchi badala ya  kuendelea  kukaa ofisini ,hivyo aliwataka idara ya maji  wilaya ya Ludewa  kujitathini kabla ya  kuwajibishwa .
Kwani alisema  kuwa  idara  hiyo mbali ya kushindwa  kuwajibika kutimiza  wajibu  wake bado katika kijiji  hicho amejitokeza mhisani  kwa ajili ya  kusaidia mradi huo na kuwaomba idara  hiyo ramani  kwa ajili ya  kuanza  utekelezaji wa mradi huo ila bado wameshindwa kuchora mchoro  huo hadi sasa kwa zaidi ya miezi sita  sasa.
"Nimezungumza na Mladea ambao ndio  wahisani  wanadai hadi  sasa bado hawajapata mchoro huo ....nimezungumza na  watu  wa idara  hiyo wanadai  kuwa bado mchoro  huo ....naomba mfikishia salamu  zangu mhandisi  wa maji  vijijini kuwa  mimi kama mbunge  na wananchi  wa kata ya Ludende hatujafurahishwa na utendaji kazi yenu "
Alisema  kuwa  wananchi hao hadi sasa  wamepata kuchangia  fedha kwa ajili ya mradi huo wa maji kiasi  cha shilingi 10,000 kila mmoja  na  wapo tayari  kujitolea  kuchimba mitaro ya kupitisha  bomba  ila watendaji  wa idara hiyo ya maji  wamekuwa  kikwazo kikubwa .
Kwa  upande  wao  wananchi  wa  kijiji  hicho cha Maholong'wa wamempongeza mbunge  huyo kwa kubaini uozo huo wa watendaji  wa idara hiyo ya maji wilaya ya Ludewa na kuwa  wao toka nchi ipate  uhuru hawajapata kuona wala kutumia huduma ya maji  safi ya  bomba  zaidi ya  kuendelea kutumia maji ya mabondeni na madimbwi ya mvua ambayo si safi na salama kwa afya zao.
Walisema  kuwa awali  walianza  kumchukia mbunge  huyo amoja na diwani  wao kwa kuwaona kama mataeli na hata  wanaoitisha  mikutano  walikuwa  wakishindwa  kufika kutokana na kuona kama wamedanganywa katika mradi huo  ila sasa wamebaini  kuwa watumishi hao  wa idara hiyo ya maji ni kikwazo na wao tayari kuungana na mbunge  wao  kutaka  wafukuzwe katika halmashauri hiyo kwa madia  kuwa si msaada  kwao.

0 comments:

Post a Comment