Na Abdulaziz Lindi
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wameazimia kuandaa
kusudio la kumshitaki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kufuatia
kutowasilisha kwa Kipindi kirefu makato wanayokatwa watumishi ambao ni
wanachama wa chama cha akiba na mikopo kwa watumishi wasio Walimu wa
Halmashauri hiyo(RUWOSCO)
Wakichangia taarifa ya Mwenyekiti wa Ruwosco katika mkutano mkuu wa
chama hicho iliyoanisha baadhi changamoto mbalimbali zinazokwamisha
chama hicho ikiwemo kutokuwasilishwa kwa makato ya watumishi mara
baada ya kutoka mishahara Hazina,Bashir Mkauchumbe,Mjumbe wa Bodi ya
Ruwosco aliemaliza muda alitoa tamko la wanachama kuhusiana na madai
hayo ili kunusuru chama hicho
Akifungua mkutano mkuu wa 3 wa chama hicho,Mwenyekiti alierejeshwa
tena kuongoza chama hicho kwa kipindi cha 3 aliwataka watumishi wa
Halmashauri hiyo Kukopa kwa Busara kulingana na kanuni za Utumishi ili
kuepuka kutokuwa na akiba baada ya Mshahara
Akifunga mkutano Mkuu huo, Mgeni rasmi ,Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo,ambae pia ni Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo
aliwaasa wanachama wa chama hicho kuongeza Ushawishi kwa watumishi
wengine wa Halmashauri hiyo ili kuongeza ufanisi huku akiwahakikishia
kufikisha katika vikao vya Uongozi wa Halmashauri kuhusiana na makato
ya wanachama yasiyowasilishwa
Mtandao huu uliwasiliana kwa njia ya simu na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo,Reubern Mfune kuhusu kusudio hilo la kufikishwa
mahakamani watumishi wake alikiri kuwepo kwa Tatizo hilo ambalo tayari
Halmashauri yake imeshalipa madeni kwa asilimia kubwa ambapo hadi sasa
chama hicho kidai Tsh Milion 3
Awali wajumbe wa mkutano mkuu huo ulimchagua tena Bw Rashid Musa
Njozi kuwa Mwenyekiti kwa kipindi cha tatu huku Bi Christina Mpwapwa
kuwa Makamu Mwenyekiti na Namson Fisoo,Ahamaid Mapua,Lucy Mmuni,Ally
Katoto,Mohamed Mapanje,Leons Mpili na Saidi Ng’itu kuwa Wajumbe wa
Bodi
0 comments:
Post a Comment