Kufuatia
kuwepo hatari ya kukatika mawasiliano ya barabara ya
Makete-Bulongwa-Mbeya kufuatia kumeguka kwa kingo za barabara karibu na
daraja la Ilolo wilayani Makete mkoani Njombe kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha wilayani hapo, wahusika wametakiwa kulichukulia
uzito suala hilo
Mtandao umeshuhudia hatari ya kumeguka kwa barabara katika eneo hilo hali
ambayo endapo haitachukuliwa hatua za haraka itasababisha barabara hiyo
kukatika na kutopitika kabisa
Kufuatia
hatari hiyo, mwandishi wa mtandao alibisha hodi ofisini kwa mkuu wa
wilaya ya Makete mh Josephine Matiro ambaye alikiri kupata taarifa za
tukio hilo ambapo aliwasiliana kwa njia ya simu na meneja wa TANROADS
mkoa wa Njombe ambao waliahidi kufika mara moja kwenye eneo hilo
Mh.
Matiro amesema anatambua adha ambayo wakazi wa makete wataipata endapo
eneo hilo litakatika na kuahidi kuendelea kulisimamia ipasavyo suala
hilo hadi litakapomalizika ili kuondoa usumbufu utakaojitokeza
Mwandishi
wa mtandao amefika eneo hilo na kukuta hatua za awali
zilizochukuliwa na TANROADS mkoa wa Njombe ambao kama walivyosema
watafika mara moja ni kweli walifika na kuzungushia alama za tahadhari
eneo hilo huku wakiendelea na hatua zaidi za kukarabati eneo hilo
CREDIT:EDDY BLOG
0 comments:
Post a Comment