Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Msigwa Akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilayani Humo
Makamu Mwenyekiti wa ccm Tanzania Bara Akiondoka Mara baada ya Kumalizika kwa Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Wilayani Wanging'ombe
Hawa ni Makatibu Kata wa ccm Katika Kata za Wilaya ya Wanging'ombe Wakijadili Namna ya Kugawiwa Pikipiki Hizo
Mzee Philip Mangula Akipiga Marufuku Kugawa zawadi Kwa Mulengo wa Kufanya Kampeni ndani ya chama
CCM
Katibu Tawala wa Wilaya ya Wanging'ombe Akisoma Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu katika Wilaya Hiyo
...................................................................>>>>>>>>>>>>>>>>...................................
Chama cha Mapinduzi CCM Nchini Kimepiga Marufuku Kwa Mwanachama Yeyote wa Chama Hicho Kupita Mitaani Kugawa Zawadi Mbalimbali Kwa Mulengo wa Kufanya Kampeni Katika Kipindi Hiki.
Aidha Imetajwa Kuwa Kufanya Hivyo ni Kukiuka Kanuni na Taratibu za Chama cha Mapinduzi Ilihali Muda wa Kampeni Haujafika.
Kauli Hiyo Imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Mzee Philip Mangula Kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Wanging'ombe na Kwamba Kitendo Hicho ni Kuudharirisha Utu wa Mwanadamu Kwani Mwenye Mamla ya Kutoa Misaada Hiyo ni Kiongozi Aliyopo Madarakani tena Kwa Kukubaliwa na Mkutano Mkuu wa CCM.
Pia Mzee Mangula Amesema Kuwa Chama hicho Hakitosita Kuwachukulia Hatua za Kinidhamu watakaobainika Kufanya Hivyo Wakati si Kiongozi.
Hatua Hiyo Imekuja Kufuatia Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Njombe Kuridhia Kutolewa Kwa Msaada wa Pikipiki 20 Kwa Makatibu Kata wa CCM Katika Kata zote za Wilaya ya Wanging'ombe Zenye Thamani ya Shilingi Milioni 38 Kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge.
Akikabidhi Pikipiki Hizo Kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa,Mbunge wa Jimbo Hilo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge Amesema Kuwa Pikipiki Hizo Zitafanya Kazi ya Chama Hicho na si Vinginevyo Kwani Ndicho Chama Kinachofanya Kazi za Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010/2015.
Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe
0 comments:
Post a Comment