Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la
Modesta mkazi wa Ludewa amefariki dunia wakati akiwa njiani akikimbizwa katika
hospitali ya Mission Ikonda kulingana na tatizo la barabara ya Makete-Njombe
kuwa mbovu
Hata hivyo Mtu huyo aliyefariki dunia
katika eneo hilo la Mang’oto wilayani Maket kulingana na tatizo la ubovu wa barabara hivyo
kusababisha kutumia muda mrefu kuvuka katika eneo korofi ambalo linakadiliwa kuwa na kilomita sita,
inasemekana kuwa hadi kufikia saa kumi na moja jioni hapo juzi hali ya wagonjwa waliokuwemo katika gari hilo
waliokuwamo walikuwa katika hali mbaya
Barabara hiyo ya Makete Njombe iliyoharibika zaidi katika eneo la Mang’oto kuanzia shule
ya sekondari Mang’oto hadi getini kutopitika hali inayopelekea wasafiri
kushindwa kushindwa kufika kwa wakati katika eneo husika
Kwa taarifa za awali Zinaonyesha kuwa
kuna wakandarasi wanakuja kufanya ukarabati ambapo nao wamekwama eneo hilo
ikiwa tatizo kubwa ni kifusi kilichosambazwa katika eneo hilo ambapo hadi
kufikia juzi ya jana magari zaidi ya 10 yalikuwa yamekwama katika eneo hilo
Kwa
upande upande wa baadhi ya watu walioweza kuzungumzia suala hilo ni pamoja na
mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia naibu waziri wa maji Dk.Binilith Satano
Mahenge ambaye alikiri kufika katika eneo hilo na kuona hali
halisi na kusema kuwa barabara hiyo ipo
chini Tanroads hivyo alifanya jitihada za kuongea nao ili kuweka kifusi kingine
katika eneo hilo na kuwatoa hofu wananchi
kuwa barabara hiyo ipo kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami na
upembuzi yakinifu unaishia mwezi wa
march mwaka 2014.
Mkuu wa wilaya ya makete Bi Josephine Matiro
akizungumzia suala hilo kwa njia ya simu kutoka Jijini Dar es salaam alikiri
kupokea taarifa hizo na kusema kuwa alipozungumza na Tanroads walisema kuwa wako wanafanya utaratibu wa
kuongea na oungozi wa kijiji cha mago wilayani hapa ili kuweza kuchukua kufusi katika kijiji
hicho.
“Engenia wakati anamwaga hicho kifusi
tulimwambia anamwaga kifusi kile wakati
msimu wa mvua umekaribia akasema kuwa
atabadilisha……….”alisema bi Matilo
Dk Kasanga ni mkazi wa kijiji cha
Tandala wilayani Makete Alisema kuwa anashangazwa na serikali kupokea barabara hiyo wakati mwanzoni tu mwa msimu wa mvua imeshanza
kusumbua.
credit.kituloblog
0 comments:
Post a Comment