baadhi ya wananchi wa kata ya Kitulo wakishiriki katika maadhimisho hayo
Na Henrick Idawa, Makete
Wananchi wilayani makete wametakiwa kupanda miti aina mbalimbali ikwemo miti ya matunda,mbao,maua na kuni kwa malengo
ili kuweza kuongeza kipato chao na
kufikia lengo lilipangwa na wilaya
katika upandaji wa miti.
Hayo yamesemwa na katibu
tawala wilaya makete bw.joseph chota kwa niaba ya mkuu wa wilaya makete katika uzinduzi upandaji wa miti wilayani hapa ambapo amesema kuwa wananchi wapande miti ya matunda ikiwemo epo ambayo itawasaidia kuinua
kipato kutokana na upatikanaji wa soko hilo kwa sasa pamoja na maua kwa ajili ya
kupendezesha mazingira
Katika hatua nyingine Bw
Chota amewasihi wananchi kujiandaa na shindano la utunzaji wa vyanzo
vya maji linaloendeshwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo mshindi atatangazwa katika kilele cha siku ya mazingira duniani ambayo inatarajia
kuazimishwa tarehe tano juni mwaka huu.
Pia katibu tawala huyo amehimiza wananchi kuwa mstari wa mbele katika suala la uhifadhi wa vyanzo vya maji ili lengo
lilopangwa na halmashauri la upandaji miti kila mwaka lifikie ambapo wilaya kwa
mwaka huu 2014 imeweka lengo la kupanda miti millioni 9.
Amesema kuwa Kauli mbiu kwa mwaka huu ni misitu ni uhai panda miti
kwanza ndio ukate mti ambapo kwa wilaya
ya makete waliweka lengo la kupanda miti
milioni tisa na jumla ya miti 8,122,275 ilipandwa na kubainisha kuwa lengo hilo
lilishindwa kufanikiwa kutokana na baadhi ya kata kutowasilisha idadi ya miti
iliyopandwa katika maeneo yao
Naye mwenyekiti wa kijiji cha
nkenja bw.zabroni chengula ameushukuru uongozi wa wilaya ya makete kwa uzinduzi
wa upandaji miti katika kata hiyo na amewasihi wananchi kupanda miti ya mbao
katika maeneo ambayo hayasitawi mazao na kulinda mifugo isiingie katika
mashamba ya watu ili kuepuka migogoro.
katika uzinduzi huo ambao
hufanyika kila mwaka tarehe kumi mwezi
januari ambapo kwa mwaka huu umefanyika katika kata ya kitulo wilayani hapa
na kuhudhuliwa na viongozi siasa,viongozi wa mashirika
binafsi,wakuu wa idara ,viongozi wa kata na kijiji na wananchi wa kijiji cha
nkenja na ujuni licha ya kuwepo kwa
changamoto ya uchache wa wananchi ulisababisha na shughuri za kiuchumi na mnada uliokuwa ukiendelea katika kata hiyo.
0 comments:
Post a Comment