Wadaiwa kuwaponya Kwa Maombi na Kutelekeza Dawa. Msafara wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Ukitokea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Njombe Leo Kuelekea Saiti.
Mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi.Fatma Mrisho Akieleza Lengo la Tume Hiyo Kufanya Ziara Ya Siku Mbili Mkoani Njombe.Baadhi ya Wanafunzi Katika Shule ya Mount Living Stone Kibena Njombe.
Hapa Baadhi ya Walimu wa Shule ya Msingi Mpechi Njombe Wakiwa na Wajumbe wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Ikizungumza na Wabafunzi Katika Shule Ya Mount Living Stone Kibena Njombe Leo
Kamishina wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Akiwawakilisha Wakristo Askofu Mstaafu Peter Mwamasika Akizungumzia Suala la Ukimwi Njombe Leo
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Akikabidhiwa Taarifa ya Sheria za Kudhibiti Ukimwi Toka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Tume Bi.Fatma Mrisho Nje ya Ofisi za Mkoa wa Njombe.
Na Gabriel Kilamlya Njombe.
Watu Waishio Na Virusi Vya Ukimwi Katika Mkoa Wa Njombe Wamewatuhumu Baadhi Ya Viongozi Wa Madhehebu Ya Dini Kupotosha Umma Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa Maombi.
Wakizungumza Mbele Ya Mwenyekiti Mtendaji Wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Tacaids Fatma Mrisho Baadhi Ya Watu Waishio Na Vvu Wamesema Viongozi Wa Dini Wamekuwa Wakiwalagai Waathirika Wa Ukimwi Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa Maombi Na Hivyo Kuacha Kutumia Dawa Na Kupunguza Makali (Arv).
Wamesema Hali Hiyo Imesababisha Baadhi Ya Waathirika Kuacha Kutumia Dawa Na Kwenda Kliniki Na Hivyo Kujikuta Katika Hatari Ya Kushambuliwa Zaidi Na Magonjwa Nyemelezi Ya Ukimwi Na Hivyo Kuhatarisha Maisha Yao.
Wakiwa Kwenye Kikao Cha Wadau Mbalimbali Wa Ukimwi Wakiwemo Wataalamu Wa Afya Katika Ukumbi Wa Halmashauriya Wilaya Ya Njombe Baadhi Ya
Waathirika Hao Wamesema Viongozi Hao Wa Dini Wamekuwa Wakichangia Watu Kuacha Kutumia Dawa Kwa Kuwadanganya Watu Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa Maombi.
Katika Hatua Nyingine Imegundulika Kuwa Baadhi Ya Waathirika Wamekuwa Wakiacha Kutumia Dawa Hizo Na Badala Yake Wanajiingiza Kwenye Matumizi Ya Pombe.
Peter Mwamasika Ni Askofu Mstaafu Wa Kanisa La Kiinjili La Kilutheri Tanzania Dayosisi Ya Dodoma Na Kamishina Wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Taifa Kwa Niaba Ya Wakristo Ambaye Amesema Kuwa Pamoja Na Viongozi Wa Dini Kupinga Matumizi Ya Kondomu Lakini Wanapaswa Kuwaelimisha Wananchi Njia Sahihi Za Kutokomeza Janga La Ukimwi.
Tume Hiyo Ilipowasili Katika Shule Ya Msingi Mpechi Ilibaini Kuwepo Kwa Upungufu Mkubwa Wa Walimu Wa Kiume Hali Iliyotajwa Kuwa Inasababisha Kushindwa
Kutolewa Kwa Elimu Ya Ukimwi Kutokana Na Usawa Wa Kijinsi,Ambapo Mmoja Wa Walimu Pekee Wa Kiume Katika Shule Hiyo Alisimama Na Kupaza Sauti Yake Akiomba Serikali Kuongeza Idadi Ya Walimu Wa Kiume Shuleni Hapo.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Mtendaji Wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi.Fatma Mrisho Amesema Kwa Kuwa Vijana Wamekuwa Wakikumbwa Na Janga La Ukimwi Kuliko Watu Wengine,Serikali Itaendelea Kuhakikisha Vijana Wanaelimishwa Ipasavyo Katika Masuala Ya Kujikinga Na Masuala Ya Ukimwi.
Tume Hiyo Ya Kudhibiti Ukimwi Imeanza Ziara Ya Kuwatembelea Wananchi Mjini Njombe Kwa Siku Mbili Ambapo Pamoja Na Mambo Mengine Imewafikia Walimu Na Wanafunzi Kwenye Shule Za Msingi Mpechi Na Mount Living Stone Ambapo Hapo Kesho Inahitimisha Ziara Hiyo Ya Siku Mbili Kwa Kutembelea Shule Za Sekondari Ili Kubaini Chanzo Cha Maambukizi Hayo.
0 comments:
Post a Comment