tg

Monday, April 7, 2014

CHANA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI NJOMBE

 NAIBU WAZIRI WA WANAWAKE JINSIA NA WTOTO DKT PINDI CHANA AKIWASILI KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI ULEMBWE
 MKUU WA CHUO CHA ULEMBWE BWANA  FRANCIS HAULE AKIWATEMBEZA WAGENI KATIKA MIRADI YA CHUO HICHO

 SAMADI YA NG'OMBE AMBAYO TAYARI IMEKWISHA KUTUMIKA KATIKA MITAMBO YA BAYO GESI


 JENERETA LA UMEME LINALOTUMIKA KWA SASA BAADA YA KUKOSEKANA KWA UMEME


 MASHINE ZA CHELEHANI KWAAJILI YA UFUNDI USHONAJI



 KAIMU AFISA MAENDELEO YA JAMII WILAYA YA WANGING'OMBE  MICHAEL HAULE
 AKISOMA TAARIFA KWA MGENI RASMI MKUU WA CHUO FRANCIS HAULE

 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI AMBAE NI WAZIRI WA WANAWAKE JINSIA NA WATOTO NA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE
WAZIRI WANAWAKE JINSIA NA WATOTO PINDI CHANA AKITOA HOTUBA YAKE AKIWA KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII ULEMBWE
Naibu waziri wa wanawake Jinsia na Watoto Pindi Chana leo ameanza ziara ya siku mbili

mkoani Njombe kwa kutembelea vikundi vya Vikoba Makambako na vyuo vya maendeleo

ya jamii Ulembwe na Njombe mjini ambapo pamoja na mambo mengine amewataka

wananchi kuwapeleka watoto wao kujiunga ili kupata elimu ya ufundi stadi ya kujitegemea

Na kujipatia ajira kwa kujiajiri.

Akizungumza akiwa katika chuo cha maendeleo Ulembwe Naibu waziri wa wanawake

jinsia na watoto Pindi Chana amewataka maafisa maendeleo kufanya kazi ya ziada kwa

kutembelea na kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo vyuo

vya ufundi stadi pamoja na kutoa elimu kwa jamii kutambua umuhimu wa kujiunga na

vyuo hivyo.

Aidha Bi.Chana amepongeza kwa hatua za maendeleo zinazofanywa na wanachuo wa

Ulembwe kwa kutoa fani  mbalimbali huku akichukua baadhi ya changamoto ambazo

zimekuwa zikivikabili  vyuo vya maendeleo ya Ufundi stadi hapa nchini na kwenda

kuzifanyia kazi ambapo amesema pamoja na changamoto hizo vyuo hivyo vinatakiwa

kubuni mbinu mbadala za kuweza kuwasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zilizo

chini ya uwezo wao.

Mkuu wa wilaya ya Njombe bi. Sarah Dumba pamoja na mambo mengine amemshukuru

waziri wa wanawake,jinsia na watoto kwa kuwatembelea na kusikiliza kero zinazowakabili

wanavyuo na vikundi vya akina mama na vituo vya watoto na kwamba huenda ikawa

mwafaka kwa mkoa wa Njombe kupelekewa misaada na kutatua baadhi ya changamoto

zinazowakabili.

Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Hosea Mpagike

amewapongeza vijana  na wazazi ambao wametambua  umuhimu wa kujiunga na vyuo

hivyo ili kupatiwa elimu ya ufundi na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwapatia uwezo wa

kujitegemea   pindi watakapo kuwa uraiani  kwa manufaa yao.

Awali akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya wananchi

Ulembwe bwana Francis Haule amesema kuwa pamoja na serikali kuhamasisha vijana

kujiunga na vyuo hivyo ili kujifunza ufundi stadi lakini bado wananchi wanamuamko

mdogo wa kupeleka watoto wao katika chuo hicho ambapo mpaka sasa kina jumla ya

wanachuo hamsini na tatu huku bado kinauhitaji mkubwa wa wanafunzi wa masomo ya

ufundi.

Aidha bwana Haule amesema kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali

ikiwemo ukosefu wa miundombinu ya umeme,upungufu wa watumishi,ukosefu wa

usafiri,huku kikifanikiwa kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo ujenzi wa

maabara,kujenga mtambo wa gesi ya samadi kwaajili ya kupikia pamoja na kutoa fani

mbalimbali za useremala,uashi,umeme wa nyumbani,ushonaji nguo,huku kikitoa masomo

ya stadi za maisha,hisabati,kiingereza,uchoraji, ujasiliamali na kompyuta.


Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho wameshukuru uongozi wa chuo cha Maendeleo

cha wananchi Ulembwe kwa jitihada mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili

kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza huku wakipongeza mkuu wa

chuo kwani amekuwa msaada mkubwa kufanikisha maendeleo ya chuo hicho kwa kutafuta

wafadhili mbalimbali kusaidia chuo hicho.

Ziara hiyo ya Naibu waziri Wanawake ,Jinsia na watoto  kesho inatarajia kuendelea katika

Wilaya ya Ludewa  ambapo leo waziri huyo ametembelea kikundi cha wanawake UCLAS

makambako ambacho kinashughulika na mikopo ya wananchi vijijini VIKOBA ambapo

lengo la ziara hiyo ni kuwasikiliza wajasiliamali,vikundi na vyuo vya maendeleo na

changamoto zake. 
NA MICHAEL NGILANGWA

0 comments:

Post a Comment