tg

Sunday, September 6, 2015

Thursday, November 20, 2014

SIMON KAHEMELE KUZIKWA LEO KIJIJINI KWAKE MBONGO

0 comments

kitambulisho chake ambacho kilikutwa katika ajali hiyo
hapa ndipo alipopata ajali hiyo kabla ya kutolewa mwili wake ambao ulibanwa na vyuma vya gari hiyo


gari iliyobeba mwili tayari kwa mazishi ikiwa katika kituo cha Polisi wilayani Ludewa kwa safari ya kuelekea Manda Mbongo
Mke wa marehemu Kahemele aliyechuchumaa akiwa na ndugu wa marehemu wakiliangalia Gari iliyosababisha kifo chake katika kituo cha polisi Ludewa
Gari iliyobeba mwili wa marehemu Simon Kahemele ikiondoka katika kituo cha polisi Ludewa mjini tayari kwa safari ya manda

Mfanyabiashara mkubwa jijini Mbeya aliyepata ajari ya gari katika mteremko wa Kimelembe karibu kabisa na migodi ya makaa ya mawe Nkomang’ombe wilayani Ludewa mkoani Njombe anatarajia kuzikwa leo katika kijiji cha Mbongo kata ya Manda.

Saturday, August 9, 2014

KAMANDA WA POLISI MKOA WA NJOMBE APATA AJALI, "BODY GUARD" WAKE AFARIKI DUNIA.

0 comments

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani.

Na James Festo, Njombe.

KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  pamoja na dereva wake Nuaka Seme  wamelazwa katika hispitari ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea  kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia  jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.

Akiongea na vyombo vya habari  huku akipatiwa matibabu katika hospitari ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP Yahaya  rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hanaruhusa Kamanda Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa nne za usiku katika barabara ya  Makambako hadi Njombe.

Aidha Jeshi la Polisi  limesema kuwa  katika ajali hiyo aliyefariki dunia ni George  Stephano  Matiko (24)

 H580 Pc George  Enzi za uhai wake.
Nuaka Sema aliyekuwa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili PT 2058  alisema kuwa kutokana  gari hilo la mizigo kukaa katikati ya barabara walishindwa kupishana kwa wakati na kuligonga kwa nyuma na baadae kukutana uso kwa uso na nguzo ya umeme iliyowasababishia ajali.

"ghafla niliona gari mbele likiwa limewasha taa zote za mbele (full light) likiwa upande wetu na nilivyoona hivyo niliwasha taa kuashiria hatari  na ndipo mwenye gari la mizigo alianza kukwepa kuelekea upande wake na wakati tukipishana mwishoni kwa kuwa lilikuwa refu tulienda tukakwanguana ndipo tulipoteza mwelekeo" alisema dereva huyo.

Aliongeza kuwa " mara baada ya kukwanguliwa tukilikwepa lori tukaigonga nguzo ya umeme na hapo hapo mwenzetu akafariki na tunashukuru sana wafanyakazi wa kampuni ya tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na lile lori hatukuweza kuchukua namba zake na liliendelea na safari".

Kwa upande wake  Afisa muuguzi wa hospitari hiyo  Bw. Denis Haule alisema kuwa majeruhi wawili  walipokelewa majira ya saa tano usiku na mwingine  alikuwa amekwisha fariki dunia na kubainisha kuwa hali ya majeruhi hao inaendelea vizuri na  Kamanda wa Polisi anaweza kuruhusiwa muda wowote.

"tumewapokea jana usiku  majeruhi  wawili na mmoja  akiwa amekwisha fariki dunia , hali yao kwa sasa inaendelea vizuri  na kamanda anaweza kuruhusiwa wakati wowote....lakini dereva wake anatakiwa kuendelea kupewa matibabu kutokana na maumivu mbalimbali katika mwili wake.

.............................MWISHO...........................

Friday, August 8, 2014

KAMATI TENDAJI YA NPC YANOLEWA.

0 comments

.Lengo ni kutaka Kuunda Kamati ya MaadiliKushoto ni Katibu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe Hamis Kasapa  Katikati ni Allan Lawa  Meneja Maadili Baraza la Habari Tanzania
Bwana Gabriel Kilamlya ambaye ni  Mtunza Hazina Msaidizi Kwenye Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe Kushoto Akiandika na kulia ni Aldo Sanga ambaye ni  mjumbe wa kamati tendaji.
Zenobia Mtei na Michael Katona Wajumbe wa kamati hiyo.
 
Lilian Mkusa kutoka shirika la Daraja ni katibu msaidizi wa chama hicho.
Wanahabari na Viongozi wa Kamati Tendaji Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe  Wakiwa Kwenye Semina ya Siku Moja Toka Baraza la Habari Tanzania MCT Mjini Njombe

Wednesday, May 7, 2014

VETA MAKETE WATEMBELEA WATOTO YATIMA NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI

1 comments


 Wafanyakazi wa VETA Makete wakiwa katika picha na watoto yatima wa kituo cha Bulongwa.
 Mfanyakazi wa VETA Makete akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituoni hapo
 Sanga akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa katika kituo cha Bulongwa
 Wakifurahia pamoja na watoto hao kwa kuimba nyombo.
 Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya kituo hicho.
 Methew Komba akiwa amembeba mtoto yatima
 watoto wakifurahia kutembelewa na wafanyakazi wa VETA Makete.
 Hapa mmoja wa wafanyakazi wa VETA Makete akicheza na watoto hao.
---------
Kufuatia wilaya ya Makete mkoani Njombe kuwa miongoni mwa wilaya zenye watoto yatima, wafanyakazi wa chuo cha VETA Makete wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Bulongwa kilichopo wilayani hapa na kutoa misaada mbalimbali

Akizungumza na mwandishi wetu kwa niaba ya wafanyakazi wenzake alioambatana nao Bw. Mathew Komba amesema wao kama VETA Makete wameguswa na namna watoto hao wanavyopata tabu kwani hawakupenda kuishi maisha hayo lakini kutokana na kufiwa na wazazi wao ndiyo maana wapo katika kituo hicho

Amesema awali walikuwa wamepanga kuwatembelea watoto hao kabla ya pasaka lakini kutokana na sababu zisizoepukika walishindwa kufanya hivyo lakini walijipanga kama walivyokuwa wamedhamiria na jana walifika kituoni hapo kuwaona watoto hao na kuwapa msaada huo

Bw. Komba amesema baadhi ya vitu walivyovikabidhi ni pamoja na mafuta ya kupikia, sukari, mchele, sabuni, juisi, dawa za meno na vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya tsh. 329,000/=

Amewaomba wadau wengine kuwaunga mkono kwa kwenda kuwasaidia watoto yatima kwani ni jukumu la jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawatunza watoto hao licha ya kwamba wanalelewa kwenye vituo mbalimbali

Kwa upande wake Bi Sekela Nkyami kutoka kituo hicho cha kulelea watoto yatima Bulongwa amesema ingawa kituo hicho kina vitega uchumi mbalimbali lakini bado kinategemea misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali wakiwemo wakazi wa Makete wenye moyo wa huruma kama walioufanya chuo cha VETA

Amesema watoto hao waliopo katika kituo hicho si mali ya kituo pekee bali ni wa jamii yote kwa hiyo kuiomba jamii kushirikiana nao katika matunzo ili watoto hao wasijisikie wapweke kutokana na uyatima walio nao

"Ni kweli uyatima unatesa, ila tunawaomba wananchi waje kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hawa, kumekuwa na kasumba kuwa wakishaletwa hapa basi si wao tena bali ni wa kituo, hii sia sawa bali tunatakiwa tushirikiane kwa pamoja chochote kidogo utakachokipata kinatosha kutusaidia" amesema Bi. Nkyami
 
  na eddy blog

Tuesday, April 8, 2014

HABARI PICHA; NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO DKT PINDI CHANA LEO AHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI MKOANI NJOMBE

0 comments


 SHANGWE NA NDEREMO ZIKIFANYIKA KUMPOKEA NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO AKIWASILI KITONGOJI  CHA  NGALAWALE MJINI LUDEWA

 HAPA NAE MHESHIMIWA YUPO KUBURUDIKA NA WANANCHI HAO KABLA YA KUINGIA KWENYE UKUMBI WA MKUTANO


 NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO AKIWA PAMOJA NA WATAALAM MBALIMBALI TOKA HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA KATIKA KITONGOJI HICHO.





 NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO DKT CHANA AKITOA HOTUBA KWA WANAKIKUNDI NA BAADHI YA WANANCHI WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO LEO


Monday, April 7, 2014

CHANA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI NJOMBE

0 comments

 NAIBU WAZIRI WA WANAWAKE JINSIA NA WTOTO DKT PINDI CHANA AKIWASILI KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI ULEMBWE
 MKUU WA CHUO CHA ULEMBWE BWANA  FRANCIS HAULE AKIWATEMBEZA WAGENI KATIKA MIRADI YA CHUO HICHO

 SAMADI YA NG'OMBE AMBAYO TAYARI IMEKWISHA KUTUMIKA KATIKA MITAMBO YA BAYO GESI


 JENERETA LA UMEME LINALOTUMIKA KWA SASA BAADA YA KUKOSEKANA KWA UMEME


 MASHINE ZA CHELEHANI KWAAJILI YA UFUNDI USHONAJI



 KAIMU AFISA MAENDELEO YA JAMII WILAYA YA WANGING'OMBE  MICHAEL HAULE
 AKISOMA TAARIFA KWA MGENI RASMI MKUU WA CHUO FRANCIS HAULE

 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI AMBAE NI WAZIRI WA WANAWAKE JINSIA NA WATOTO NA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE
WAZIRI WANAWAKE JINSIA NA WATOTO PINDI CHANA AKITOA HOTUBA YAKE AKIWA KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII ULEMBWE
Naibu waziri wa wanawake Jinsia na Watoto Pindi Chana leo ameanza ziara ya siku mbili

mkoani Njombe kwa kutembelea vikundi vya Vikoba Makambako na vyuo vya maendeleo

ya jamii Ulembwe na Njombe mjini ambapo pamoja na mambo mengine amewataka

wananchi kuwapeleka watoto wao kujiunga ili kupata elimu ya ufundi stadi ya kujitegemea

Na kujipatia ajira kwa kujiajiri.

Akizungumza akiwa katika chuo cha maendeleo Ulembwe Naibu waziri wa wanawake

jinsia na watoto Pindi Chana amewataka maafisa maendeleo kufanya kazi ya ziada kwa

kutembelea na kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo vyuo

vya ufundi stadi pamoja na kutoa elimu kwa jamii kutambua umuhimu wa kujiunga na

vyuo hivyo.

Aidha Bi.Chana amepongeza kwa hatua za maendeleo zinazofanywa na wanachuo wa

Ulembwe kwa kutoa fani  mbalimbali huku akichukua baadhi ya changamoto ambazo

zimekuwa zikivikabili  vyuo vya maendeleo ya Ufundi stadi hapa nchini na kwenda

kuzifanyia kazi ambapo amesema pamoja na changamoto hizo vyuo hivyo vinatakiwa

kubuni mbinu mbadala za kuweza kuwasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zilizo

chini ya uwezo wao.

Mkuu wa wilaya ya Njombe bi. Sarah Dumba pamoja na mambo mengine amemshukuru

waziri wa wanawake,jinsia na watoto kwa kuwatembelea na kusikiliza kero zinazowakabili

wanavyuo na vikundi vya akina mama na vituo vya watoto na kwamba huenda ikawa

mwafaka kwa mkoa wa Njombe kupelekewa misaada na kutatua baadhi ya changamoto

zinazowakabili.

Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Hosea Mpagike

amewapongeza vijana  na wazazi ambao wametambua  umuhimu wa kujiunga na vyuo

hivyo ili kupatiwa elimu ya ufundi na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwapatia uwezo wa

kujitegemea   pindi watakapo kuwa uraiani  kwa manufaa yao.

Awali akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya wananchi

Ulembwe bwana Francis Haule amesema kuwa pamoja na serikali kuhamasisha vijana

kujiunga na vyuo hivyo ili kujifunza ufundi stadi lakini bado wananchi wanamuamko

mdogo wa kupeleka watoto wao katika chuo hicho ambapo mpaka sasa kina jumla ya

wanachuo hamsini na tatu huku bado kinauhitaji mkubwa wa wanafunzi wa masomo ya

ufundi.

Aidha bwana Haule amesema kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali

ikiwemo ukosefu wa miundombinu ya umeme,upungufu wa watumishi,ukosefu wa

usafiri,huku kikifanikiwa kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo ujenzi wa

maabara,kujenga mtambo wa gesi ya samadi kwaajili ya kupikia pamoja na kutoa fani

mbalimbali za useremala,uashi,umeme wa nyumbani,ushonaji nguo,huku kikitoa masomo

ya stadi za maisha,hisabati,kiingereza,uchoraji, ujasiliamali na kompyuta.


Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho wameshukuru uongozi wa chuo cha Maendeleo

cha wananchi Ulembwe kwa jitihada mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili

kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza huku wakipongeza mkuu wa

chuo kwani amekuwa msaada mkubwa kufanikisha maendeleo ya chuo hicho kwa kutafuta

wafadhili mbalimbali kusaidia chuo hicho.

Ziara hiyo ya Naibu waziri Wanawake ,Jinsia na watoto  kesho inatarajia kuendelea katika

Wilaya ya Ludewa  ambapo leo waziri huyo ametembelea kikundi cha wanawake UCLAS

makambako ambacho kinashughulika na mikopo ya wananchi vijijini VIKOBA ambapo

lengo la ziara hiyo ni kuwasikiliza wajasiliamali,vikundi na vyuo vya maendeleo na

changamoto zake. 
NA MICHAEL NGILANGWA