Capt.Mstaafu Asseri Msangi,akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sarah Dumba mwishoni kulia ni mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi wakiwa kwenye kikao cha Utekelezaji wa Ilani mkoa wa Njombe.
TAARIFA YA MAFANIKIO
YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM KUANZIA
MWAKA 2005 – 2012 ILIYOSOMWA NA MKUU WA MKOA MHESHIMIWA KAPT. (MSTF) ASERI
MSANGI
Ndugu
Wananchi;
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kutufikisha kuuona Mwaka Mpya wa 2013 tukiwa wazima na Afya njema.
Pili napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu
za dhati kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe pamoja na Wadau wa Maendeleo kwa
kushiriki kwao kwa namna mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za Maendeleo
na Utoaji wa huduma Mkoani kwetu. Hotuba
yangu leo inahusu Mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa
kipindi cha 2005 – 2012.
Ndugu Wananchi;
Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005 na
2010, Wananchi wa Mkoa wa Njombe wamefanya shughuli mbalimbali za Kiuchumi na
Kijamii. Aidha, shughuli kuu ni pamoja
na Kilimo, Ufugaji, Upasuaji wa Mbao, Uvuvi, Biashara, Ajira za Maofisini na
Viwandani. Sambamba na shughuli hizi, usimamizi na ufuatiliaji katika Mamlaka
za Serikali za Mitaa umeimarishwa ili kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi
zinaboreshwa. Mafanikio yaliyopatikana
katika sekta mbalimbali ni kama ifuatavyo:-
1.0 UTAWALA BORA
Ndugu Wananchi;
(i) Maeneo Mapya ya Utawala
Mnamo tarehe
1 Machi 2012 Serikali
ilitangaza rasmi kuanzishwa kwa Mkoa wa Njombe ukitokea Mkoa wa Iringa na kutangaza katika Gazeti la Serikali Toleo Namba
9 la mwaka 2012. Sanjari na
kuundwa Mkoa, Serikali ilitangaza kuanzishwa
kwa Wilaya ya Wanging’ombe ikitokea
katika Wilaya ya
Njombe. Aidha, Serikali ilianzisha Halmashauri ya
Mji wa Njombe katika mwaka 2007
na mwezi Julai 2012 Halmashauri
ya Mji wa Makambako ilianzishwa.
Taratibu za kisheria zinaaendelea ili
kuweza kuanzisha Halmashauri
ya Wilaya ya
Wanging’ombe. Aidha, idadi ya
Kata na vijiji vimeongezeka. Kuanzishwa kwa maeneo haya mapya ya utawala ni
mafanikio makubwa yenye nia ya kusogeza
huduma karibu zaidi na wananchi.
(ii)
Mapambano Dhidi ya Rushwa
Serikali
imeendelea kufuatilia na kuhakikisha kwamba stahili zote za watumishi zinalipwa
kwa wakati ili wasiingie kwenye vishawishi vya kutaka kutoa au kupokea
rushwa. Aidha, haki na stahili za utoaji
huduma zimeainishwa katika mabango na mbao za matangazo ili wananchi wafahamu
stahili zao. Pia elimu inaendelea kutolewa kuhusu athari za rushwa mahali pa
kazi. Yote haya ni katika kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora na
Serikali inakuwa wazi kwa wananchi wake.
(iii)
Uboreshaji wa Mishahara na stahili nyingine
za Watumishi
Kwa
kipindi cha mwaka 2005 – 2012, Serikali imekuwa ikiboresha mishahara na stahili
mbalimbali za watumishi ikiwa ni pamoja na kuwapandisha vyeo kwa wakati, kuwajengea
uwezo kwa kuwapa mafunzo na kuwawezesha kupata mikopo mbalimbali katika Taasisi
za Fedha.
(iv) Mapambano Dhidi ya UKIMWI Sehemu za Kazi
Serikali
ya Awamu ya nne imeendelea kuwahudumia watumishi wanaojitokeza kuwa
wameathirika na Virusi vya UKIMWI. Watumishi
hao wanahudumiwa kwa matibabu na lishe. Ili
kufanikisha hili Serikali imetoa Waraka wa Watumishi wa Umma Na.1 mwaka 2007
ukitoa maelekezo kwa waajiri wote kuhusu
utoaji wa huduma kwa watumishi hao.
(v) Mpango wa Maboresho katika
Sekta ya Utumishi wa Umma
Serikali
imefanya maboresho ya Utumishi wa Umma kwa awamu mbili. Katika Mpango huu mifumo mbalimbali
imeboreshwa ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa Umma ili waweze
kutoa huduma bora kwa wananchi. Aidha,
vitendea kazi vimeweza kupatikana kupitia Mpango huu ambapo utendaji kazi
katika Ofisi mbalimbali za Serikali umeimarika.
(vi) Vikao Mbalimbali vya Kisheria
Vikao
mbalimbali vya Kisheria vimeendelea kufanyika, hili imesaidia kupunguza
malalamiko kwa wananchi. Pia katika maeneo ya kazi kuhakikisha kuwa vikao vya Watumishi na
Waajiri vinafanyika mara kwa mara ili kupunguza malalamiko ya Watumishi sehemu
za kazi lengo likiwa ni kuboresha huduma kwa Wananchi. Aidha, Mabaraza ya
Wafanyakazi yameundwa na yanafanya kazi.
(vii) Kushughulikia Malalamiko Mbalimbali
Madawati
ya malalamiko yameanzishwa sehemu za kazi katika Ofisi zote za Serikali ili
kupokea na kushughulikia malalamiko mbalimbali yanayowasilishwa na wananchi. Sanjari
na hili masanduku ya maoni yamewekwa katika sehemu za utoaji huduma ili kupata
maeneo yenye udhaifu na kuyaboresha.
2.0 SEKTA YA KILIMO
Ndugu Wananchi;
Mafanikio makubwa
yameonekana katika Sekta ya Kilimo na hivyo kuboresha uchumi na maisha ya
Wakulima. Maeneo yaliyoonesha ufanisi ni pamoja na:-
(i) Wananchi wameendelea kupokea pembejeo za
kilimo kwa njia ya ruzuku ambapo utaratibu huu umefanikisha upatikana wa
pembejeo kwa urahisi na kuongeza tija. Katika kufanikisha mpango huu Serikali
imetoa ruzuku ya pembejeo za kilimo zenye thamani ya jumla ya shilingi
36,166,982,000 hadi sasa, kiasi hicho cha fedha kimeweza kuwanufaisha wakulima
kulima ekari 520,011 za mazao ya Mahindi
na Mpunga.
(ii) Uzalishaji
wa mazao ya Chakula na Biashara
umepanda
na kufikia tani
1,155,45,
kwa mwaka 2012 ikilinganishwa na tani 463,694 mwaka 2005.
Hii
ni kutokana na kuongezeka kwa tija ya uzalishaji ambapo kwa Mahindi
uzalishaji tija uliongezeka kutoka wastani wa tani 2 kwa hekta hadi kufikia
wastani wa tani 3 kwa hekta, Mpunga kutoka wastani wa tani 1.5 kwa hekta
hadi kufikia wastani wa tani 2.5 kwa hekta, Ndizi kutoka wastani wa tani
uzalishaji tija uliongezeka kutoka wastani wa tani 2 kwa hekta hadi kufikia
wastani wa tani 3 kwa hekta, Mpunga kutoka wastani wa tani 1.5 kwa hekta
hadi kufikia wastani wa tani 2.5 kwa hekta, Ndizi kutoka wastani wa tani
8.5 kwa hekta hadi
kufikia wastani wa tani 13 kwa hekta na viazi
mviringo
kutoka tani 11 kwa hekta hadi kufikia wastani
wa tani 15 kwa hekta.
(iii) Kwa miaka yote saba Mkoa umeendelea kuwa na
ziada ya mazao ya chakula
na
kuwa na usalama wa Chakula Mkoani. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka
2011/12
Mkoa una ziada ya tani 500,135 za nafaka na tani 222,345 za
viazi
Mviringo
na Mihogo.
(iv) Eneo linalolimwa limeendelea kuongezeka mwaka hadi
mwaka na kufikia
Ha.367,769 ambazo ni sawa
na asilimia 98 ya malengo kwa mazao ya
chakula na Ha. 76,971 sawa na asilimia 99 kwa mazao ya Biashara
ikilinganishwa na Ha. 232,212 za mazao ya chakula na Ha. 17,645
za mazao
ya biashara katika mwaka 2005.
(v) Skimu za umwagiliaji
zilizoendelezwa/zilizoboreshwa zimeongezeka ambapo
mwaka 2005 kulikuwa
na skimu 2 zilizoendelezwa na hadi kufikia mwaka
2012 Mkoa una skimu 7 zilizoendelezwa
zenye wastani wa eneo hekta 2,194
zinazofaa kwa umwagiliaji.
(vi) Huduma za ugani zimeboreshwa
kwa kuongeza idadi ya
Maafisa Ugani
ambapo mwaka 2005 walikuwa
Maafisa Ugani 172 na hadi kufikia mwaka
2012 Mkoa una jumla ya Maafisa Ugani 363, aidha
katika vijiji ambavyo
havina Maafisa Ugani, Wagani Kazi
240 wamepewa mafunzo na kufanya
huduma za ugani vijijini ambapo Wagani
kazi hao hawakuwepo mwaka
2005.
(vii) Matumizi
ya zana za kilimo yameongezeka kama inavyooneshwa kwenye
jedwali hapa chini:-
jedwali hapa chini:-
AINA YA ZANA
|
IDADI YA ZANA
MWAKA 2005
|
IDADI YA ZANA MWAKA
2012
|
ASILIMIA YA
ONGEZEKO
|
Trekta kubwa
|
163
|
209
|
128.2%
|
Trekta za mikono
(Powertillers)
|
0
|
164
|
100%
|
Plau
|
1,504
|
2,098
|
139.5%
|
Maksai
|
17,776
|
33,867
|
190.5%
|
Mkokoteni
|
973
|
1,013
|
104.1%
|
Mashine za kupandikiza
Mpunga (Rice transplanters)
|
0
|
2
|
100%
|
Mashine ya kuvuna (combine
harvester)
|
1
|
3
|
300%
|
3.0 SEKTA YA MIFUGO:
Ndugu Wananchi;
(i) Idadi ya
Mifugo imeongezeka katika
kipindi cha mwaka
2005 hadi 2012 kama
ifuatavyo:-
AINA YA MIFUGO
|
IDADI YA MIFUGO
MWAKA 2005
|
IDADI YA MIFUGO MWAKA
2012
|
Ng’ombe
|
151,307
|
171,482
|
Mbuzi
|
44,464
|
96,295
|
Kondoo
|
34,613
|
35,600
|
Kuku
|
978,564
|
11,896,175
|
Nguruwe
|
10,863
|
83,756
|
(ii) Miundombinu ya Mifugo imekarabatiwa na kujengwa
kama ifuatavyo:-
MAELEZO
|
IDADI
|
|
2005
|
2012
|
|
Majosho
|
54
|
82
|
Machinjio kubwa
|
3
|
6
|
Machinjio ndogo
|
4
|
10
|
Malambo
|
14
|
51
|
Mabanda ya Ngozi
|
4
|
8
|
(iii) Udhibiti wa Magonjwa mbalimbali ya Mifugo
kwa kutumia chanjo na uogeshaji
umeongezeka na kufanya maambukizi ya
magonjwa kupungua kama ifuatavyo:-
MAGONJWA
|
2005
|
2012
|
Magonjwa yaenezwayo na
kupe
|
80%
|
25%
|
Mdondo wa Kuku
|
40%
|
25%
|
Chambavu na Kimeta
|
15%
|
5%
|
Kichaa cha Mbwa
|
5%
|
1%
|
Homa ya Mapafu ya Ng’ombe
|
5%
|
0%
|
Minyoo
(Ng’ombe, Mbuzi na Nguruwe)
|
45%
|
15%
|
(iv) Uzalishaji wa mazao ya mifugo umeongezeka
kama ifuatavyo:-
MAZAO
|
2005
|
2012
|
Maziwa (Lita)
|
1,524,312
|
2,202,826
|
Mayai
|
987,435
|
1,871,388
|
Jibini Kilo
|
8,456
|
13,201
|
Ng’ombe wanaouzwa
|
5,675
|
10,001
|
4.0 USIMAMIZI KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA
MITAA
Ndugu Wananchi;
(i)
Ukaguzi wa Hesabu za Halmashauri:
Kwa
kipindi cha mwaka 2005 – 2011, Halmashauri zimekaguliwa na Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na hati mbalimbali zimetolewa kama
ifuatavyo:-
MWAKA
|
NJOMBE
TC
|
NJOMBE
DC
|
LUDEWA
DC
|
MAKETE
DC
|
2005/2006
|
-
|
Yenye mashaka
|
Hati safi
|
Hati safi
|
2006/2007
|
-
|
Yenye mashaka
|
Yenye mashaka
|
Hati safi
|
2007/2008
|
Hati safi
|
Yenye mashaka
|
Hati safi
|
Hati safi
|
2008/2009
|
Hati safi
|
Yenye mashaka
|
Hati safi
|
Yenye mashaka
|
2009/2010
|
Hati
yenye mashaka
|
Yenye mashaka
|
Hati safi
|
Yenye mashaka
|
2010/2011
|
Hati safi
|
Hati safi
|
Hati
yenye mashaka
|
Yenya mashaka
|
(ii)
Uboreshaji, Udhibiti na Ufuatiliaji wa
Taarifa za Fedha za Umma kwenye
Halmashauri
Mkoa
umepatiwa Mtaalamu Mshauri anayeshughulikia masuala ya fedha, ukaguzi na mifumo
ya fedha, Mtaalamu huyo anashirikiana na Wataalam wa Sekretarieti katika
kuboresha usimamizi wa fedha, ukaguzi, ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za
Matumizi ya fedha za umma kupitia utekelezaji wa Miradi mbalimbali katika
Halmashauri. Pia vitengo vya Ukaguzi wa ndani vya
Halmashauri vimepatiwa magari na
Kompyuta ili kurahisisha utendaji
kazi na utoaji wa Taarifa za Ukaguzi kwa wakati.
Mkoa una programu ya kuzijengea uwezo Halmashauri
katika matumizi ya rasilimali watu na mali inayoendeshwa chini ya Programmu ya
Shirika lisilo la Kiserikali la Tunajali
kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID). Programu hii
inaziwezesha Halmashauri kutoa huduma kwa viwango na itasaidia kuzipatia hati
safi za ukaguzi wa Hesabu ili ziweze kuendelea kufuzu kupata fedha za ruzuku za Mamlaka za Serikali za Mitaa (Local
Government Development Grant LGDG).
(iii)
Kupeleka Madaraka kwa
Wananchi:
Mkoa
umesimamia kwa karibu ugatuaji wa Madaraka kwa Wananchi chini ya mfumo wa (D by
D). Mipango yote ya huduma za Kijamii na
Kiuchumi kupangwa kuanzia ngazi ya Kitongoji, Kijiji, Kata hadi ngazi ya Halmashauri, ambayo
huwasilishwa ngazi ya Mkoa na baadaye Taifa. Baada ya kupitishwa mipango hiyo
utekelezaji na Tathmini hufanyika katika ngazi za kijiji. Aidha fedha za utekelezaji hupelekwa ngazi za kijiji
chini ya usimamizi wa Halmashauri na Mkoa.
5.0 SEKTA YA ELIMU:
Ndugu Wananchi;
Serikali
imeendelea kuboresha Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi na Elimu ya Sekondari; ikiwa
ni pamoja na elimu ya ufundi na elimu ya juu. Aidha, wananchi wameendelea
kushirikishwa na kuhamasishwa katika kuandikisha watoto kwenda shule, kusimamia
mahudhurio, kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na ujenzi
wa Shule za Msingi na Sekondari.
Mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na:-
(i) Elimu
ya Awali imepanuliwa kwa kiasi kikubwa kwani mwaka 2005 kulikuwa na wanafunzi
15,538 wa elimu ya awali na hadi kufikia mwaka 2012 kumekuwa na wanafunzi
51,767 sawa na ya ongezeko la asilimia 70%. Hii ina maana kuwa madarasa ya
elimu ya awali yameongezeka kutoka madarasa 206 yaliyokuwepo mwaka 2005 hadi
madarasa 365 yaliyopo mwaka 2012.
(ii) Kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi wa darasa la
saba kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi
mwaka. Mwaka 2005 kiwango cha ufaulu kilikuwa 63% na 2012 kiwango kimepanda na
kufikia asilimia 74.5% sawa na ongezeko la asilimia 11.5%. Lengo la Mkoa ni
kufikia asilimia 85% ifikapo 2015.
(iii) Serikali
imeweka msukumo wa uandikishaji
wa wanafunzi wenye umri wa
miaka 7 – 13 katika elimu
ya msingi. Kwa mfano uandikishaji wa watoto
wanaoanza darasa la
kwanza umekuwa katika wastani wa asilimia 99% toka
mwaka 2005 hadi mwaka 2012.
(iv) Serikali
imeendelea kujenga na kupanua
miundombinu ya shule za msingi
kama vile nyumba za walimu na madarasa. Kwa
mfano mwaka 2005, kulikuwa
na shule
za msingi 432
na mwaka 2012 kuna
shule 472. Kwa upande wa
madarasa ya shule za
msingi, mwaka 2005, kulikuwa na madarasa
2,340, na
kufikia mwaka 2012, kumekuwa na madarasa
3,264. Nyumba za walimu pia
zimeongezeka kwa asilimia
22.1% yaani kutoka nyumba 1,660
zilizokuwepo
mwaka 2005 kufikia nyumba 2130
zilizopo mwaka 2012.
(v) Kwa upande wa uandikishaji wa wanafunzi
wenye ulemavu, Shule Maalum za
Msingi zilizopo zimeendelea kuboreshwa ili
kutoa huduma bora kwa Wanafunzi
wenye ulemavu na mahitaji maalum. Shule hizi zimeongezeka kutoka shule
mbili zilizokuwepo mwaka 2005 hadi shule nne
zilizopo sasa.
(vi) Kwa upande wa
shule za sekondari kumekuwepo na ongezeko la shule za
sekondari ili kuwezesha kila kata
kuwa na shule moja. Mwaka 2005 kulikuwa
na shule za sekondari 52 na hadi
kufikia mwaka 2012, kumekuwepo na shule
za sekondari 102. Mkoa wa Njombe
una kata 96.
(vii)
Kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza. Mwaka
2005 wanafunzi walioingia kidato cha kwanza walikuwa asilimia 63% ya
wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi. Na mwaka 2013
wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza watakuwa asilimia 74.5 ya wale
waliofanya mtihani huo.
(x)
Mkoa
umeongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na masomo ya
kidato
cha 5 – 6
kwa kuongeza idadi ya
shule za kidato
cha 5 – 6 kutoka shule
moja iliyokuwepo
mwaka 2005 hadi shule 15 za masomo
hayo zilizopo
mwaka 2012.
(xi)
Nyumba za Walimu kwa shule za Sekondari
zimeendelea kujengwa kutoka
nyumba 205 zilizokuwepo
mwaka 2005 hadi nyumba
458 zilizopo
mwaka 2012. Jitihada
zinafanyika za kufikia lengo la
nyumba 1,407.
(xii)
Kwa upande wa madarasa
ya shule za
sekondari nayo yameongezeka
kutoka madarasa 269
yaliyokuwepo mwaka 2005 hadi madarasa 990
yaliyopo mwaka 2012.
(xiii) Kwa upande
wa Walimu wa shule
za Msingi kumekuwepo
na ongezeko
la ajira.
Mwaka 2005 kulikuwa na Walimu
2,709 na
mwaka 2012 kuna
Walimu 3,700. Hapa kuna ongezeko
la Walimu 1,091 sawa na asilimia 73.
(xiv) Vyuo vinavyotoa mafunzo ya ualimu pia
vimeongezeka Mkoani kwani mwaka 2005 kulikuwa na chuo kimoja cha ualimu na
mwaka 2012 kuna vyuo viwili vinavyotoa mafunzo hayo.
(xv)
Walimu wa shule za
Sekondari nao wameongezeka kwa asilimia 76, yaani kutoka Walimu
304 waliokuwepo mwaka
2005 hadi Walimu 1,281 waliopo mwaka 2012
(xvi) Kwa
upande wa vyuo vikuu na vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi, mwaka 2005
hapakuwepo Chuo Kikuu Mkoani, lakini kufikia mwaka 2012 Mkoa umepata matawi
mawili ya kutolea elimu ya juu, na kuna vyuo vitano vya kutolea mafunzo ya
ufundi.
Pamoja
na mafanikio hayo, serikali mkoani inaendelea kuhamasisha jamii, watu binafsi
na mashirika ya dini kuwekeza katika elimu kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya
juu na ufundi.
6.0.
SEKTA
YA AFYA
Ndugu Wananchi;
Mafanikio
yaliyopatikana katika Sekta ya Afya ni kama ifuatavyo:-
(i)
Mwaka 2005 Mkoa
wa Njombe ulikuwa
na Hospitali 10, Vituo vya Afya 19 na Zahanati 116, hadi
Mwaka 2012 Mkoa una
jumla ya Hospitali 10, Vituo vya Afya 21
na Zahanati 152. Hivyo
vituo
vya kutolea huduma vimeongezeka kutoka
146 mwaka 2005 hadi 183 mwaka 2012 sawa na ongezeko la asilimia 25.3, kama ifuatavyo:-
1.0.
Mgawanyo wa Huduma za Afya na wamiliki Mwaka
2005.
HUDUMA ZA AFYA
|
MMILIKI
|
WILAYA
|
JUMLA
|
||
Njombe
|
Ludewa
|
Makete
|
|
||
Zahanati
|
1. Serikali
|
40
|
33
|
13
|
86
|
2. Binafsi/Shirika
|
17
|
3
|
10
|
30
|
|
JUMLA
|
57
|
36
|
23
|
116
|
|
Vituo vya Afya
|
1. Serikali
|
3
|
3
|
3
|
9
|
2. Binafsi
|
6
|
3
|
1
|
10
|
|
JUMLA
|
9
|
6
|
4
|
19
|
|
Hospitali
|
1. Serikali
|
1
|
1
|
1
|
3
|
2. Binafsi
|
3
|
2
|
2
|
7
|
|
JUMLA
|
4
|
3
|
3
|
10
|
|
JUMLA
|
1. Serikali
|
44
|
37
|
17
|
98
|
JUMLA
|
2. Binafsi
|
26
|
9
|
13
|
48
|
|
JUMLA
|
70
|
46
|
30
|
146
|
1.1.
Mgawanyo wa Huduma za Afya na Umiliki kwa
Mwaka 2012:
HUDUMA ZA AFYA
|
MMILIKI
|
WILAYA
|
|
JUMLA
|
||
Njombe
|
Njombe TC
|
Makete
|
Ludewa
|
|
||
Zahanati
|
1. Serikali
|
42
|
22
|
13
|
39
|
116
|
2. Binafsi/Shirika
|
14
|
6
|
12
|
4
|
36
|
|
Vituo vya Afya
|
1. Serikali
|
4
|
1
|
3
|
3
|
11
|
2. Binafsi/Shirika
|
1
|
5
|
1
|
3
|
10
|
|
Hospitali
|
1. Serikali
|
0
|
1
|
1
|
1
|
3
|
2. Binafsi
|
2
|
1
|
2
|
2
|
7
|
|
JUMLA
|
1. Serikali
|
46
|
24
|
17
|
43
|
130
|
2. Binafsi
|
17
|
12
|
15
|
9
|
53
|
|
JUMLA
YOTE
|
1. Serikali na
Mashirika/Binafsi
|
63
|
36
|
32
|
52
|
183
|
Hivyo,
Mkoa una jumla ya Hospitali 10, kati yake 3, ni za Serikali, 6 za Mashirika ya
Dini na 1 ya shirika binafsi. Vipo vituo vya afya 21, kati yake 11 ni vya Serikali
na 10 vya Mashirika ya Dini. Pia tunazo
Zahanati 152, Kati ya 116 za Serikali, 31 za Mashirika ya Dini na 5 watu
Binafsi.
(ii)
Katika
kipindi cha mwaka 2005 na 2012, idadi ya akina Mama wajawazito wanaojifungulia
katika vituo vya kutoa huduma imeongezeka. Mwaka 2005 ilikuwa asilimia 56, na
Mwaka 2012 kiwango kimeongezeka na kuwa asilimia ipatayo 89.
(iii)
Kwa Mujibu wa taarifa ya Vifo vya watoto
wachanga (infants Mortality rate (IMR) na watoto chini ya miaka 5 (under 5
mortality rate (U5MR), navyo vimepungua. Mwaka 2005 kulikuwa na vifo 25 kwa
kila watoto 1,000 waliozaliwa hai, ambapo kwa mwaka 2012 vifo vilifikia 17 kati
ya watoto 1,000 waliozaliwa hai.
(iv)
Idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua
kutoka vifo 250 kwa kila akina mama 100,000 mwaka 2005, hadi kufikia vifo 109
kwa kila akina mama 100,000 mwaka 2012.
(v)
Aidha,
kiwango cha chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja kimeongezeka
kutoka asilimia 87 kwa Mwaka 2005 hadi kufikia Asilimia 91 kwa Mwaka wa 2012.
(vi)
Suala la ugonjwa wa UKIMWI limekuwa
likishughulikiwa kwa ushirikiano na Wadau mbalimbali wakielekeza katika Kutoa
Elimu ya VVU, Ushauri Nasaha na Kupima kwa hiari. Hadi mwaka 2012 kuna jumla ya
Vituo vya kutolea dawa za kupunguza makali ya UKIMWI vipatavyo 36 tofauti na
Mwaka 2005 ambapo kulikuwa na Vituo 6 tu.
7.0 SEKTA YA MAJI:
Ndugu Wananchi;
Katika
kipindi cha awamu ya nne huduma ya maji katika Mkoa wa Njombe imeongezeka
toka 54.15% mwaka 2005 hadi 61.9% mwaka
2012, sanjari na mafanikio haya ya miradi ya maji, miradi ya maji inaendelea
kujengwa katika maeneo mbalimbali ili kuboresha huduma kwa wananchi.
Aidha
kwa kipindi hiki mifuko ya maji imefikia kiasi cha shilingi 319,695,459.59, kamati
za maji 294,na vyombo huru vya watumiaji maji 13.
Hali
ya huduma ya maji inategemewa kuongezeka mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa
miradi ya maji inayofadhiliwa na Benki
ya Dunia kama ifuatavyo:-
Na.
|
WILAYA
|
MRADI
|
MFADHILI
|
MAELEZO
|
1
|
MAKETE
|
Ubiluko,
Mpangala, Matamba, Mbela, Mlondwe na Ng’onde
|
Benki
ya Dunia (WSDP)
|
Miradi
ifuatayo inaendelea kujengwa; Ubiluko, Mpangala, Matamba ‘ Mbella,
|
2
|
LUDEWA
|
Ilininda,
Mbwila, Lugarawa na Lumbila
|
Benki
ya Dunia (WSDP)
|
Ilininda , Mbwila ,
|
3
|
NJOMBE
VIJIJINI
|
Masaulwa,
Image, Ihang’ana, Kifumbe na Wangama
|
Benki
ya Dunia (WSDP)
|
Masaulwa,
Image, Ihang’ana ,
|
4
|
NJOMBE
MJI
|
Lugenge,
Kisilo, Utalingolo, Limage, Igominyi, Madobole,
Njoomlole, Luponde, Magoda, Madope (Ludewa
DC) na Luvuyo
|
Benki
ya Dunia (WSDP)
|
Lugenge, Kisilo, Utalingolo, Limage na
Igominyi .
|
Aidha kwa baadhi ya miradi
inayojengwa, mifumo ya uvunaji maji ya mvua itajengwa kama mfano ili wananchi
waweze kjifunza na hatimaye waweze kujenga kwenye miji yao.
Utunzaji
Wa Mazingira
Kuna sheria za utunzaji wa
Mazingira zinazotumiwa na Vijiji ili kuhifadhi vyanzo vya maji na Mazingira kwa
ujumla. Sheria hizi ni pamoja na Sheria
ya mazingira ya mwaka 2004 Na. 20 kifungu cha 57 kifungu kidogo cha 1, sambamba
na Sheria ya maji Na. 11 na 12 ya mwaka 2009 zinazolinda mazingira na vyanzo
vya maji.
8.0 HALI YA BARABARA
Ndugu Wananchi;
Mkoa
una Barabara jumla ya Km.5, 521.26 ambazo zimegawanyika katika Halmashauri na
“TANROADS” kama ifuatavyo:-
Mji
wa Njombe Km.1,248, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Km. 1,476.6, Halmashauri ya
Wilaya Ludewa Km. 1,055 na Halmashauri ya Wilaya Makete Km. 619.05 na TANROADS
ina jumla ya Kilomita 1,123.26.
Barabara
za Lami zilikuwa hazipo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo kwa kipindi
hiki jumla ya Km. 16 zimejengwa kwa mgawanyo ufuatao:-
Ludewa
Km.1.5, Halmashauri ya Mji Njombe Km.2 na Makete Km.12.50 na Kilomita 2
zimeanza kujengwa katika Wilaya mpya ya Wanging’ombe.
Mnamo
Mwaka wa fedha 2005/2006 – Mgao wa Mfuko wa Barabara na fedha za Maendeleo
ilikuwa na Jumla ya Shilingi 2.1 Bilioni, kwa Halmashauri ya Wilaya Njombe,
Makete, Ludewa na Tanroads.
Hali
ya kupitika kwa barabara za vijijini imeboreshwa na kufikia hatua ya kupitika
kwa asilimia zifuatazo:-
(i) Njombe Mji toka asilimia 50 hadi 85%
(ii) Halmashauri ya Wilaya Njombe toka asilimia 40
hadi 75%
(iii) Halmashauri ya Wilaya Ludewa toka asilimia 35
hadi 75%
(iv) Halmashauri ya Wilaya Makete toka asilimia 30
hadi 55%
(v) Wakala wa barabara TANROADS toka asilimia 60
hadi 95%
Hali
hii imepelekea wastani wa upitikaji wa Barabara zote za Changarawe, Udongo na
Lami kuwa Asilimia 77 Ki-Mkoa.
Serikali
imeendelea kuimarisha Mfuko wa Barabara “Road fund” na fedha za maendeleo ili
kuongeza kasi ya Ukarabati na ujenzi wa Miundombinu. Fedha za kuhudumia
Barabara zimeendelea kuongezeka ambapo Mwaka wa fedha 2012/2013 Jumla ya
Shilingi 16.7 Bilioni zimepangwa kutumika Mkoani ambapo Halmashauri zimetengewa
Shilingi 5.0 Bilioni na Wakala wa Barabara (TANROADS) Shilingi 11.7 Bilioni.
Nishati ya Umeme
Idadi
ya wateja wanaotumia umeme kwa ujumla, katika Mkoa wa Njombe ni asilimia 18. Aidha
miradi inayoendelea ya kuunganishia wateja inayofadhiliwa na REA pamoja na
miradi ya TANESCO ni 65.
Miradi
yote kwa ujumla tunategemea kuongeza wateja kwa asilimia 8, na hivyo kupelekea
kufikia asilimia 26 mpaka 30, ifikapo Mwaka 2015, ikiwa ndio lengo la Serikali kuhakikisha Watanzania wanaotumia nishati ya umeme kufikia
asilimia 30.
9.0 SEKTA YA MISITU
Ndugu Wananchi;
Sekta
ya misitu imeendelea kukua kwa kipindi chote kuanzia mwaka 2005 hadi 2012. Mwaka
2005 Mkoa ulikuwa na jumla ya hekta 311,736 hadi kufikia hekta 505,990 za
misitu kwa mwaka 2012. Hili ni ongezeko la asilimia 162 ambapo eneo hili ni
misitu ya kupandwa na ya asili.
Mafanikio katika sekta ya misitu ni kama
ifuatavyo:-
Ongezeko
la ukubwa wa eneo lililopandwa miti kutoka Hekta 137,390 kwa mwaka 2005 hadi Hekta 207,421 kwa mwaka 2012, hii ni
sawa na ongezeko la asilimia 151
I.
Hifadhi ya misitu ya vijiji kutoka hekta 87,920 kwa mwaka 2005 Hadi hekta 124,025 kwa
mwaka 2012 sawa na ongezeko la asilimia 141.Ongezeko hili ni kutokana na
ushirikishwaji wa wananchi katika usimamizi wa misitu.
II.
Uvunaji wa misitu ya kupandwa kwa matumizi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara ya mazao ya misitu yaani mbao
umeongezeka kutoka mita za ujazo 317,874 mwaka 2005 hadi mita za ujazo 601,342
mwaka 2012 za mbao sawa na ongezeko la asilimia 189.2, nguzo kutoka mita za
ujazo 1,372 mwaka 2005 hadi 3,952 mwaka 2012 sawa na ongezeko la asilimia 288.
III.
Mapato yatokanayo na misitu imeongezeka
kutoka shilingi bilioni 254. 4 mwaka 2005 hadi shilingi bilioni 481.5 mwaka
2012, hili ni ongezeko la asilimi 189.3. Kwa kiasi kikubwa Mkoa wa Njombe
umekuwa unazalisha mazao ya misitu kwa wingi ambayo yanatumika ndani ya
Mkoa, Mikoa mingine na Nje ya mipaka ya
Tanzania. Hali hii huchangia pato la kaya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
IV.
Matukio
ya uchomaji moto yamepungua kutoka matukio 345 mwaka 2005 hadi 158 mwaka 2012.
Hii ni kutokana na wananchi kujengewa uwezo wa kutambua na kuthamini umuhimu wa
kutunza mazingira kwa kutumia sheria ndogo za vijiji na Halmashauri zilizopo.
.Kwa
kutambua umuhimu wa sekta ya misitu kiuchumi na hifadhi ya mazingira, serikali
imeendelea kusimamia na kuhamasisha wananchi na taasisi mbalimbali kuhusu upandaji
wa miti katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa.
10.0 SEKTA
YA NYUKI
Ndugu Wananchi;
Mwitikio
wa Wananchi katika kutekeleza shughuli za ufugaji wa Nyuki ni mkubwa ambapo
Mkoa una jumla ya mizinga 56,315 na uzalishaji wa asali na nta umeongezeka
ikilinganishwa na mwaka 2005 kama ifuatavyo:-
(i)
Uzalishaji
wa asali umeongezeka kutoka lita 23,262 mwaka 2005 hadi lita 223,823 mwaka 2012
sawa na asilimia 962.
(ii)
Uzalishaji
wa nta umeongezeka kutoka kilo 690 mwaka 2005 hadi kilo 33,025.4 mwaka 2012
sawa na asilimia 4,786 kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo.
Zao
|
Mwaka
|
Thamani (Shilingi)
|
Mwaka
|
Thamani (Shilingi)
|
Onezeko la uzalishaji %
|
|
2005
|
|
2012
|
|
|
Asali
(lita)
|
23,262
|
58,155,000
|
223,823
|
1,678,672,500
|
962
|
Nta
(Kg)
|
690
|
1,035,000
|
33,025.4
|
247,690,500
|
4,786
|
Aidha
Mkoa una wajasiriamali wadogowadogo wapatao 6 ambao hujishughulisha na shughuli
za kufungasha asali. Hamasa inaendelea kutolewa kwa wawekezaji ili waweze
kujitokeza kuwekeza katika sekta hii muhimu kiuchumi na kimazingira.
11.0 SEKTA
YA USHIRIKA:
Ndugu Wananchi;
Hali
ya Vyama vya Ushirika imeendelea kuimarika hasa Vyama vya Kuweka na Kukopa
(SACCOS) ambavyo vimeongezeka kutoka 52 katika mwaka 2005 hadi 90 mwaka 2012.
Aidha,
Idadi ya Wanachama na Mitaji imeongezeka kutoka wananchama 8,367 na mitaji ya Shilingi 2,694,536,767
katika mwaka 2005 na kufikia wanachama 37,719 na mitaji ya Shilingi 17,972, 219,029 katika mwaka huu wa 2012.
Vyama
vya Mazao (AMCOS) vimeongezeka kutoka 53 mwaka 2005 na kufikia 80 mwaka 2012.
Aidha, mitaji imekua kutoka Shilingi 15,194,619 na kufikia Shilingi 24,860,271.
Idadi ya wanachama imeongezeka kutoka 3,484 mwaka 2005 na kufikia 7,187 mwaka
2012.
12. CHANGAMOTO NA UFUMBUZI
Ndugu Wananchi;
Pamoja na mafanikio haya makubwa niliyoyaelezea,
zipo changamoto chache ambazo tunaendelea kuzipatia ufumbuzi ili kuendelea
kuboresha maisha ya wananchi. Baadhi ya changamoto hizo ni kama ifuatavyo:-
·
Upatikanaji wa maji
safi na salama katika baadhi ya maeneo ya Mjini (Mji wa Njombe) na baadhi ya
maeneo ya vijijini (Tarafa ya Wanging’ombe). Serikali inaendelea kufuatilia
upatikanaji wa ufumbuzi wa changamoto hii kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
·
Upatikanaji wa soko
la uhakika la mazao ya kilimo hasa
viazi mviringo na matunda. Mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Bashara imeanza
kulitafutia ufumbuzi suala hili kwa
kuandaa mpango wa ujenzi wa soko la
Kimataifa litakalojengwa katika Mji wa Makambako katika kipindi hiki cha
Serikali ya awamu ya Nne. Aidha Mkoa unaendela kuwahamasisha wakulima
kuimarisha Vyama vyao vya Ushirika wa Mazao ili waweze kuwa na nguvu ya pamoja
katika kupanga bei na kuuza mazao yao kwa bei nzuri.
·
Upatikanaji wa
ruzuku ya pembeo za kilimo kwa zao la viazi mviringo ambalo ni chanzo kikubwa cha uchumi wa wananchi wa Mkoa
wa Njombe. Mkoa unaendelea kuishawishi Wizara husika
kufikiria uwezekano wa kutoa ruzuku katika zao la viazi.
13. HITIMISHO:
Ndugu wananchi;
Napenda
kuwahakikishia kuwa Mkoa utaendelea kusimamia shughuli za Ulinzi na Usalama ili
Wananchi waweze kufanya shughuli zao za Kiuchumi na Kijamii bila kuwa na
mashaka yoyote. Wananchi wanasisitizwa
waendelee kuongeza juhudi na maarifa katika shughuli za uzalishaji mali.
Aidha,
ninaomba Wananchi waongeze juhudi za ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari
ili watoto wote waliofaulu darasa la saba mwaka jana (2012) waweze kuingia
kidato cha kwanza katika mwaka 2013.
Ndugu
Wananchi niwatakie tena Heri ya Mwaka Mpya katika mwaka 2013.
“MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU UBARIKI
MKOA WETU MPYA WA NJOMBE”.
0 comments:
Post a Comment