Bw. Issa Ngumba. |
Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera anayefanyia kazi wilayani Kakonko mkoani Kigoma Bw. Issa Ngumba aliyepotea katika mazingita tata amekutwa amekufa na kunyofolewa sehemu zake za siri
Taarifa kutoka Kigoma ambazo mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com umezipata hivi punde zinadai kuwa mwili
wa mwanahabari huyo umekutwa nje kidogo na mkoa wa Kigoma.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma RPC Kishai amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuwa bado jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi zaidi .
Mbunge wa jimbo la Kigoma Zitto Kabwe pia amepata kuzungumza na
mtandao huu na kudai kuwa ameguswa na kifo cha mtangazaji huyo na
kutaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya kifo
chake.
Pia Kabwe ameeleza jinsi ambavyo mwanahabari huyo alivyoweza
kuifanya kazi yake kwa jamii ya Kigoma kwa ufanisi zaidi na kuwa wakati
mwingine yeye kama mbunge alikuwa akizunguka na mwanahabari huyo katika
jimbo lake.
" Kweli nimeguswa sana na kifo cha kusikitisha cha mwanahabari huyo
nilimfahamu vema kwa utendaji kazi wake ila nawapa pole sana
waandishi wote nchini kwa msiba huu mkubwa .....na zaidi nitapata
kueleza mengi mara baada ya uchunguzi"
Taarifa za awali
zilizotolewa na Jeshi la Polisi wilayani Kakonko baada ya kupotea kwa
mwanahabari huyo zilisema kuwa Bw Ngumba alipotea tangu
January 05 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mke wake Bi.
Rukia
Yunus kuwa anakwendwa Muhange senta wilayani Kakonko na kwamba hajarudi
nyumbani hadi sasa.
Kufuatia
tukio hilo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Muhange
wanaendelea kumtafuta katika mapori ya kijiji hicho baada ya rafiki zake
kueleza kuwa aliwaanga kuwa anakwenda kutafuta dawa msituni.
Bw. Issa Ngumba. |
Aidha jeshi
la polisi Wilayani Kibondo liliomba kampuni za mitandao ya simu anayotumia Bw
Ngumba kusaidia kutambua simu zake zilipotumika kwa mara ya mwisho ili
kurahisisha upatikanaji wake.
0 comments:
Post a Comment