SIRI nzito imeibuka sakata la diwani wa kata ya Ifunda jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa mheshimiwa Elia Mgwila (CCM) pichani anayedaiwa kufumaniwa na mke wa mtu na kupigwa kisha kukatwa sikio moja na kung'olewa meno matatu .
Diwani huyo ambae kwa siku ya jana mara baada ya kutoka zahanati ya Misheni Masumbo Ifunda kwa matibabu alirejeshwa nyumbani kwake eneo la Ifunda Kibaoni ila hadi sasa inasadikika amekuwa akiishi kwa kujifungia ndani ya nyumba yake ili kukwepa kuonana na wapiga kura wake ambao wamekuwa wakifika kumpa pole.
Mbali ya diwani huyo kuchagua maisha ya kujificha kwa wapiga kura wake pia inadaiwa kabla ya kufumaniwa diwani huyo alionywa vya kutoshwa na jemba huyo mwenye mke kuacha kamchezo hako kabaya ka kujisogeza kwa mama watoto wake ila alikana kuwa hana mahusiano na wala hamtambui mwanamke huyo.
Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wasiri wa nyeti hiyo wanadai kuwa diwani huyo ameonywa zaidi ya mara mbili na mmiliki halali wa mwanamke huyo Bw Daima Msigala ila alipuuza na kumtolea maneno ya vitisho mwenye mke huyo akimtaka kuacha kumchafulia jina lake .
Hata hivyo imeelezwa kuwa diwani huyo dowezi mara kadhaa mkewe alifuma ujumbe mfupi katika simu yake ya kiganjani ukitoka kwa mwanamke huyo mke wa Msigala Bi Lucy Lalika wakipangana jinsi ya kuonana na kupongezana kwa jinsi ambavyo walivyofanikiwa kusaliti ndoa zao kwa kuivunja amri ya sita ila kila alipofuatwa na kulalamikiwa juu ya hilo aliruka futi 100 .
Jambo lililopelekea mwenye mali Bw Msigalla ambae ni fundi uashi kuweka mtego kwa kudanganya kuwa anakwenda kikazi Mafinga na ndipo bila kufikiria mheshimiwa na mwanamke huyo waliamua kukutana kwa ndoa ya muda yaani ndoa ya usiku ndani ya chumba cha mwenye mali umbali wa mita kama 100 kutoka nyumbani kwa mheshimiwa diwani na kuamua kuivunja amri ya sita kabla ya mwenyewe kurejea na kutembeza kichapo na kumcharanga sikio moja diwani huyo asiyesikia la mkuu kisha kumtoa meno matatu na kumweka alama ya kumcharanga mapanga miguuni kabla ya wananchi kufika kumpelea kutibiwa huku akiwa amefungwa kamba miguu na mikono kama kibaka sugu.
Wakati huo huo jitihada za kumpata diwani huyo bado zinaendelea na nyumbani kwake na nyumbani kwa mwenye chake wote wakiwa wamefunga milango yao na wapiga kura kutoka pande zote za kata ya Ifunda wakikusanyika nje ya nyumba yake kutaka kumpa pale bila mafanikio.
Habari hii inaendelea endelea kufuatilia mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com utapata ukweli wa mambo
0 comments:
Post a Comment