Bw. Limbakisye Shimwela akiwa na baadhi ya makombe ya tuzo mbalimbali za ushindi katika ofisi yake.
Madiwani hayo walitoa baraka hizo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo na kuhudhuriwa mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu ambae alikuwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Peter Tweve alisema kuwa ombi ambalo limeombwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya fedha hizo zilizorejeshwa linaungwa mkono na madiwani na kumtaka mkurugenzi kuelekeza feddha hizo ambazo zilikuwa ni fedha za OC kwenda kutumika katika shughuli hizo za kimaendeleo .
mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Limbakisye Shimwela aliwataja watumishi waliohusika na wizi wa fedha hizo na kusimamuishwa kazi kuwa ni pamoja na Willium Fwimi ,Alan
Leonard, Paulo Mwaluko wote wakiwa ni watumishi idara ya uhasibu.
Aidha
Shimwela amewataka watumishi wote kuwa na nidhamu katika kazi na
uaminifu katika fedha, ili kufanikisha mpango wa kuleta maendeleo ya
wananchi na taifa kwa ujumla.
“Hakuna
kitu kizuri katika kazi kama kuwa muumini wa uadilifu, unajua unapopewa
dhamana si kama wale wengine wasio na cheo kama chako hawana akili au
hawana uwezo huo, bali Mungu amependa tu wewe kuwa hivyo, kwa hiyo
unatakiwa kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa ili kujenga imani kwa
wananchi unaowatumikia,” Alisema Shimwela.
Amesema
fedha za idara ya elimu msingi shilingi Milioni 45 zitachonga
madawati 600 ambayo yatagharimu shilingi Milioni 27, kwa shule 20,
huku kila shule ikipatiwa madawati 30.
Huku shule Milioni
18 zitakarabatiwa miundombinu ya barabara kwa shule 6 ambazo zimekuwa
kikwazo kikubwa kwa wanafunzi na walimu kufika shuleni, na kujenga
nyumba ya mwalimu iliyokuwa imenguka katika shule ya msingi Nandala.
Ambapo
shule za sekondari zitaboreshewa maabara 8 (Mobil Laboratories)
zitakazogharimu jumla ya shilingi Milioni 48 ili kuwawezesa wanafunzi wa
masomo ya Sayansi kufanya vizuri kwa kupatiwa mafunzo kwa vitendo.
Na
milioni 7 ikikamilisha Bweni la wanafunzi wa sekondari ya Ilogombe na
Milioni 8 zikipelekwa katika idara ya afya na hivyo gharama ya shughuli
hizo kukamilisha jumla ya shilingi Milioni 109 ya fedha zote ambazo
zilikuwa zimeibwa.
Hata
hivyo wananchi wameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo, ukiongozwa
na kusimamiwa na Mkurugenzi wake Bw. Limbakisye Shimwela kwa kufanikisha
fedha hizo kurejeshwa na hivyo kuchangia shughuli za maendeleo na
uchumi.
Wizi
huo wa kitaalamu uliofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya
kifedha hapa nchini (NMB) ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, kwa
kushirikiana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,
na kuchepusha fedha za Halmashauri hiyo zaidi ya Shilingi Milioni 109
kwa manufaa yao binafsi.
Wakizungumzia
sakata hilo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mufindi, kilichokaa kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo,
pamoja na wizi wa fedha hizo, ambapo Madiwani walisema licha ya
watumishi hao kurudisha fedha hizo lakini taratibu za kisheria
zinapashwa zichukuliwe dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine.
Akichangia
hoja ya fedha hizo za Umma, Evaristo Luhunga diwani wa Kata ya Ikweha
alisema watumishi hao wanatakiwa kupewa adhabu licha ya kurejesha fedha
hizo, kwani wamechangai kudumaza uchumi wa Halmashauri na wananchi wake.
“Hatua
hii tuliyofikia inadhihirisha wazi juu ya kazi kubwa tulioyoifanya
katika kufuatilia fedha hizi, lakini nisingependa tuishie hapa,
kwani watumishi wengi wamekuwa wakicheza na fedha za umma, lakini nini
madhara ya wizi wa fedha hizi za wananchi, kuna haja ya kuwachukulia
hatua za kisheria, ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia
kama hizi,” Alisema Luhunga.
Naye
Ernei Nyeho diwani wa Kata ya Mdabulo amesema inapotokea fedha
zilizopitishwa na baraza la madiwani kwa ajili ya kukamilisha miradi
mbalimbali halafu watu wachahe kwa maslahi yao binafsi wanachukua, watu
hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
“Mimi
katika Kata yangu fedha hizi zililenga kuboresha mradi wa elimu na afya
kwa kununua madawati pamoja na kujenga madarasa, lakini siyo tu kwenye
kata yangu, tatizo hili limeyumbisha uchumi wa Halmashauri nzima,”
Alisema Nyeho.
0 comments:
Post a Comment