tg

Saturday, February 8, 2014

MNEC WILAYA YA WANGING'OMBE ATEKELEZA AHADI YAKE YA KUTOA MIFUKO YA SARUJI UKOMOLA KIJOMBE,NJOMBE


Hiyo ni Mifuko ya Saruji Iliyotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Nebchad Msigwa.
 MNEC Huyo Akitoa Msaada wa Kalamu na Madaftari Kwa Wanafunzi Hao Jana. 
 
Na Gabriel  Kilamlya Wanging'ombe
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Wilayani Wanging'ombe Nebchad  Msingwa Ametoa Msaada wa Mifuko 11 ya Saruji Yenye Thamani ya Shilingi Laki Moja na Sitini na Tano Elfu Kwa Ajili ya Ukarabati wa Darasa na Ofisi Katika Shule ya Msingi Ukomola.

Akiongea Wakati wa Kukabidhi Msaada Huo Msigwa Amesema ni Utekelezaji wa Ahadi Yake Aliyoitoa Kwa Ajili ya Kusaidia Ukarabati Katika Shule ya Msingi Ukomola Ambayo Inakabiliwa na Upungufu wa Vyumba Vya Madarasa na Ofisi Ili Kukabiliana na Upungufu Uliopo Shuleni Hapo.

Akizungumza Mara Baada ya Kupokea Msaada Huo Diwani wa Kata ya Kijombe Nashon Kilamlya Amesema Msaada Huo wa Muifuko Kumi  na Mmoja Itasaidia Katika Ukarabati  Shuleni Hapo Ambapo Mifuko 45 Ilikuwa Inahitajika Kwa Ajili ya
Shughuli za Ukarabati.

Diwani Nashoni Amesema Kukamilika Kwa Ukarabati wa Darasa Katika Shule Hiyo Utasaidia Kumaliza Msongamano wa Wanafunzi Katika Darasa Moja na Kuongeza Kuwa Ukarabati Huo Unatarajia Kukamilika Mwezi Juni Mwaka Huu,.

Katika Hatua Nyingine Diwani Nashon Amewaomba Wananchi na Wadau wa Maendeleo Katika Kata Hiyo Kuendelea Kuchangia Miradi ya Maendeleo Ili Kusongeza Huduma za Kijamii Karibu na Wananchi.

Pamoja na Kutolewa Kwa Msaada Huo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Wilaya ya Wanging'ombe Lakini Pia Ametumia Fursa Hiyo Kuwaona Watoto Yatima Wanaosoma Katika Shule ya Msingi Korinto Pamoja na Kuwapa Zawadi ya Madaftari na Kalamu.

0 comments:

Post a Comment