Aliyekuwa
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe Maro Chacha
Ambaye Kwa Sasa Amehamishiwa Katika Mkoa wa Ilala Jijini Dar es Salaam
Amezungumza na Mtandao Huu Jinsi Alivyoipokea Taarifa ya Kuhamishwa
Mkoani Njombe.
Kamanda Maro Licha Kupokea Kwa Furaha Kubwa Taarifa ya Kuhamishiwa Mkoani Ilala Dar es Salaam Kwa Uhamisho wa Kawaida Lakini Amesema Kuwa Mipango Yake Imeshavurugika.
Pamoja na Mambo Mengine Amewataka Wananchi Wa Njombe Kumsamehe Kwa Pale Wanapoona Aliwakosea Kwani Ilikuwa ni Katika Utekelezaji wa Majukumu Yake Kwa Mujibu wa Sheria.
Aidha
Kamanda Chacha Amewaomba Wakazi wa Njombe Kumpa Ushirikiano wa Dhati
RTO Atakayefika Kama Walivyompa Yeye Kwani Mjenga Nchi ni Mwananchi
Mwenyewe.
Pia Amesema Kwa Kuwa Mkoa wa Njombe ni kati ya Mikoa Mipya Yenye Changamoto Nyingi Hivyo Jamii ni Lazima Ikubali Kutoa Ushirikiano na Viongozi Mbalimbali wa Mkoa Ili Kufanikisha Dhima Nzima ya Kimaendeleo Mkoani Njombe.
0 comments:
Post a Comment