tg

Sunday, June 2, 2013

HIVI NDIVYO MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE ALIVYOMWONYESHA KINANA JINSI ANAVYOKUBALIKA KWA WANANCHI WAKE


7
Mbunge wa Ludewa Ndugu Deo Filikunjombe akinyanyuliwa juu juu na wapiga kura wake kata  ya Lupingu mbele ya katibu mkuu  wa  CCM Taifa ndugu Abdulrahman Kinana na katibu  wa idara ya Itikadi na uenezi Nape Nnauye kama ishara ya kuwaonyesha viongozi hao jinsi wanavyomkubali mbunge  wao kutokana na kazi kubwa anayoifanya katika jimbo hilo huku wakiimba Jembe! Jembe.

8
Mbunge wa Ludewa Ndugu Deo Filikunjombe akiongea na wapiga kura wake katika kata ya Lupingu ,huku  wakiwataka  wanaoafiki CCM kupokea kata  hiyo kutoka kwa diwani wa upinzani wa TLP mwaka 2015 wanyoshe juu mikono yao ili katibu mkuu Kinana aone na kuwa iwapo  wanampenda mbunge basi  wasimchanganyie diwani

9 

Nape Nnauye Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi wa kata ya Lupingu
  10 




Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Kanali Mstaafu Abdulrahaman Kinana akitembelea na kukagua fukwe za ziwa Nyasa katika mwambao wa kata ya Lupingu Wilayani Ludewa, Kanali mstaafu Kinana amewatoa hofu wananchi wa kata ya Lupingu na kuwaambia kwamba vueni na kuishi bila wasiwasi kwani vita hakuna, mazungumzo yanaendelea vizuri na hakutakuwa na vita na mtumie rasilimali za nchi zilizopo ili mpate fedha na kujipatia kipato ili kukuza uchumi wenu na taifa kwa ujumla, katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na maneno kadhaa ambapo nchi ya Malawi imekuwa ikidai ziwa Nyasa ni mali yake, Katika picha Kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na wengine kutoka kushoto wanaoongozana na Abdulrahman Kinana ni Pindi Chana Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa Bw. Kolimba, Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo Filikunjombe na Kange Lugola Mbunge wa jimbo la Mwibara mkoani Mara CCM
5 
Mbunge wa Mwibara Kange Lugola akisakata ngoma na mmoja wa wacheza ngoma wa kikundi cha sanaa cha Lupingu

0 comments:

Post a Comment