>...Majeruhi wawili wakmibizwa Hospitali ya Ikonda Makete.
Mwili wa Marehemu Linus Nziku mkazi wa Mdasi Wanging'ombe ukiwa Umefunikwa na Kuondolewa Katikati ya
Barabara alipogongwa.
Mwendesha Baiskeli Marehemu Linus Nziku[45] aliyegongwa na Kufariki Papo hapo leo Asubuhi Katika Eneo la Nyaugao Mpakani Mwa Kijiji cha Makoga na Mdasi.
Na Gabriel Kilamlya.
Mtu Mmoja Amefariki Dunia na Wengine Wawili Wamejeruhiwa Katika Ajali ya Pikipiki Iliotokea Leo Asubuhi Katika Kijiji Cha Mdasi Kata ya Makoga Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe.
Wakizungumza na Kituo Hiki Baadhi ya Mashuhuda wa Ajali Hiyo Akiwemo Diwani wa Kata ya Makoga Bw Abraham Chaula Amesema Ajali Hiyo Imetokea Leo Katika Barabara Kuu ya Njombe - Makete.
Amemtaja Mtu Aliefariki Kwenye Ajali Hiyo Kuwa ni Linus Nziku Mkazi wa Kijiji Cha Mdasi na Kusema Kuwa Majeruhi Wawili Wamekimbizwa Katika hospitali ya Ikonda Kwa Matibabu Zaidi.
Aidha Pamoja na Kuelezea Mazingira ya Tukio Hilo,Bw Chaula Amewashauri Watumiaji wa Vyombo Vya Usafiri Hasa Pikipiki Kuwa Makini Wanapokuwa Barabarani.
Jeshi la Polisi Limethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo.
................................................................................................
0 comments:
Post a Comment