tg

Saturday, July 20, 2013

WALIOPISHA ENEO LA UJENZI WA MAKAO MAKUU WANGING`OMBE KUPEWA MASHAMBA MENGINE.

 Huyu ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chalowe ambaye ameagizwa na Mbunge Kuwapa Mashamba wananchi waliopisha Eneo la Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging:ombe.

 Naibu waziri wa Ujenzi akiagiza SERIKALI YA kijiji cha Chalowe Kuwapa Mashamba Wakulima waliopisha Eneo la Ujenzi wa MAKAO MAKUU ya Wilaya ya Wanging`ombe.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge Ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi ameuagiza Uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Chalowe Kata ya Igwachanya kuwapa Mashamba ya Kulima wananchi waliopisha Eneo la Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Kitongoji cha Wangama.

Agizo Hilo amelitoa jana wakati wa Ziara yake katika Kitongoji Hicho ikiwa ni Muendelezo wa Ziara Jimboni kwake na Kwamba kitendo cha Wananchi Kukubali kutoa Eneo Hilo kwa ajili ya Ujenzi Huo ni Jambo la Busara Hivyo kama serikali ya Kijiji inapaswa kuwaonesha eneo Jingine la Kulima haraka Iwezekanavyo.

Awali wananchi hao wamesema walishatoa Ombi la Kupatiwa eneo Jingine kwenye Ofisi ya Kijiji hadi Kwa Mkuu wa Wilaya lakini Jambo Hilo halikutekelezwa hali iliyopelekea Mbunge Huyo kuagiza Kuwashughulikia

wananchi Hao ili kuanza Ujenzi Haraka.

Jafary Gidion ni Mwananchi wa Kitongoji cha Wangama ambaye  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa  Wakulima Hao Katika eneo yatakakojengwa makao makuu ya Wilaya Hiyo,hapa akasimama na Kupaza sauti yake kwa Mbunge kwa Niaba ya Wakulima Juu ya Eneo Hilo.

Mbunge Lwenge alipofika katika Kijiji cha Igwachanya ambako ndiko Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe akakutana na Maswali Mbalimbali ya Wananchi Likiwemo la Kutaka Kupewa Ufafanuzi Juu ya Kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa Bungeni iliyoeleza Juu ya Kuwapiga Raia watakao leta usumbufu kwa Jeshi la Polisi.

 Mbunge Lwenge akizungumza na Wananchi wa Kitongoji cha Wangama Leo
 Hawa ni wananchi wa Kitongoji cha Wangama Kijiji cha Chalowe waliohoji juu ya Wao kutoa Eneo la Ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Wilaya ya Wanging`ombe Bila Kupewa Mashamba Mengine.

Hapa ni Igwachanya karibu na Ofisi za Kata ya Hiyo.

Wananchi wa Kijiji cha Igwachanya wakisikiliza Majibu ya Mbunge wao Baada ya Kumuuliza Maswali kadha wa kadha.

Na Gabriel Kilamlya.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge Ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi ameuagiza Uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Chalowe Kata ya Igwachanya kuwapa Mashamba ya Kulima wananchi waliopisha Eneo la Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Kitongoji cha Wangama.

Agizo Hilo amelitoa jana wakati wa Ziara yake katika Kitongoji Hicho ikiwa ni Muendelezo wa Ziara Jimboni kwake na Kwamba kitendo cha Wananchi Kukubali kutoa Eneo Hilo kwa ajili ya Ujenzi Huo ni Jambo la Busara Hivyo kama serikali ya Kijiji inapaswa kuwaonesha eneo Jingine la Kulima haraka Iwezekanavyo.

Awali wananchi hao wamesema walishatoa Ombi la Kupatiwa eneo Jingine kwenye Ofisi ya Kijiji hadi Kwa Mkuu wa Wilaya lakini Jambo Hilo halikutekelezwa hali iliyopelekea Mbunge Huyo kuagiza Kuwashughulikia wananchi Hao ili kuanza Ujenzi Haraka.

Jafary Gidion ni Mwananchi wa Kitongoji cha Wangama ambaye  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa  Wakulima Hao Katika eneo yatakakojengwa makao makuu ya Wilaya Hiyo,hapa akasimama na Kupaza sauti yake kwa Mbunge kwa Niaba ya Wakulima Juu ya Eneo Hilo.

Mbunge Lwenge alipofika katika Kijiji cha Igwachanya ambako ndiko Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe akakutana na Maswali Mbalimbali ya Wananchi Likiwemo la Kutaka Kupewa Ufafanuzi Juu ya Kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa Bungeni iliyoeleza Juu ya Kuwapiga Raia watakao leta usumbufu kwa Jeshi la Polisi.

Kufuatia Swali hilo Lwenge akasimama na kutolea Majibu ambapo hata yeye akarudia Kauli hiyo na Kusema"hata mimi na Sema Pigeni"

Kauli hiyo ameitoa kutokana na Kwamba Waziri Mkuu alieleza Hivyo kwa Kuwa Tayari Baadhi ya Wananchi Mtwara walishaingia Vitani wakiwa na Silaha kwa Kuchoma Madaraja,KUCHOMA Nyumba za Viongozi na Hivyo Bila Mapigano kwa silaha isingewezekana.

Ziara Hiyo Kesho inaendelea Katika vijiji Vinne vya Kata ya Ulembwe na Makoga kabla ya Kuhitimisha Julai 19 Mwaka Huu.

0 comments:

Post a Comment