Mkuu wa wilaya ya makete bi Josephine Matiro
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya makete wamelalamikia utendaji mbovu wa watendaji wa vijiji na kata ambapo zaidi ya watendaji ishirini waliopo katika kata ishirini na mbili wamedaiwa kujihusisha na unywaji pombe hali inayopelekea kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Wakitaja majina ya watendaji na hali utendaji wao wa kazi madiwani katika kikao cha robo ya nne ya mwaka 2012/2013 wamasema kuwa pamoja na upungufu wa watumishi hao lakini waliopo wana matatizo mbalimbali yakiwemo ulevi na utoro wa kuto kukaa katika vituo vyao vya kazi hadi kusababisha kushindwa kukusanya mapato na kuiingizia hasara halmashauri hiyo.
Pia katika baraza hilo wakiendelea kutoa malalamiko hayo wamesema kuwa katika kata zao kuna upungufu wa watumishi hao ishirini na moja na watumishi wengine waliopungufu ni maafisa mifugo na kilimo.
kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw Idd Nganya amekiri kuwepo kwa upungufu huo na kusema kuwa uuondoshwaji wa watumishi hao bila taarifa katika sehemu zao za kazi bila taarifa kwa baadhi ya viongozi wakiwemo madiwani katika kata zao
Pia mkurugenzi mtendaji huyo amewataka madiwani hao kuacha tabia ya kuwakataa baadhi ya viongozi wakiwemo wanaohamishwa kutokana na matatizo wanayokutwa nayo katika vituo vyao vya awali.
Aidha Baraza hilo lililoishia hapo jana limepitisha waraka wa kuwafukuza kazi watumishi nane wa sekta mbalimbali wakiongozwa na wauuguzi na maafisa ugani kutokana na tatizo la utoro wa muda mrefu
Baraza hilo pia limemchagua Aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Jison John mbalizi kuendelea kushikiria wadhifa huo sambamba na uchaguzi wa kamati mbili na wenyeviti wao.
0 comments:
Post a Comment