tg

Wednesday, December 19, 2012

FILIKUNJOMBE ACHAGULIWA KWA KURA ZA KISHINDO UJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAIFA KUTOKA WILAYANI


Bw Deo Filikunjombe
katibu  wa CCM mkoa  wa Njombe Hosea Mpangike
 Mbunge wa  jimbo la Njombe Magharibi na naibu waziri wa ujenzi Bw Greyson Lwenge akiwa na mbunge wa Makete na naibu waziri wa maji Dr Binilith Mahenge ( kulia)


Wajumbe  wa mkutano  mkuu  wa Halmashauri ya  mkoa  wa Njombe  wamemchagua  kwa kura  za  kishindo mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe  kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa  toka wilaya  ya Njombe baada ya kupata  kura 37 kti ya  kura 45 zilizopigwa katika uchaguzi  huo wa wajumbe wa kamati ya siasa ya  mkoa  wa Njombe..
Akitangaza matokeo hayo  katibu  wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpagike alisema kuwa katika wilaya ya Ludewa  kulikuwa na  wagombea  watatu katika nafasi hiyo akiwemo mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Ludewa  Matei Kongo aliyepata  kura 25 na Damiani Mwapinga aliyepata kura 24 na  hivyo  wajumbe  wawili  walioshinda ni mbunge Filikunjombe na Kongo.
Wakati  katika  wilaya ya  Wanging'ombe  Anaupendo Gombela aliyepata  kura 36 na Happiness Bomba aliyepata  kura 31 ndio walioshinda  nafasi hiyo  huku mwenyekiti  wa  Halmashauri ya  wilaya ya  Wanging'ombe Edsoni Msigwa akishindwa vibaya katika nafasi  hiyo  kwa  kupata kura 21.

0 comments:

Post a Comment