tg

Sunday, January 20, 2013

WANANCHI MJINI NJOMBE WALALAMIKIA MIUNDIMBINU DUNI YA MADARAJA


Diwani wa kata ya Njombe Mjini Lupyana Fute na mwakilishi wa halmashauri kuu ya ccm Taifa wilaya ya Njombe.

Wananchi wa Mtaa wa Kihesa na Mgendela Mjini Njombe Wamelalamikia Hali Mbaya ya Miundombinu Iliopo Kwenye Mtaa Huo Likiwemo Daraja la Linalounganisha Kati ya Mitaa Hiyo na Maeneo Mengine Kwa Kusema Kuwa Hali Yake ni Mbaya na Linaweza Kusababisha Madhara Kwa Wananchi Endapo Halitafanyiwa Marekebisho Haraka.

Wakizungumza na Uplands Fm,Baadhi ya Wananchi Hao Wamesema Licha ya Kuwasilisha Malalamiko Yao Kwa Muda Mrefu Katika Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe na Viongozi Wengine Akiwemo Diwani Lakini Bado Kumekuwa Hakuna Utatuzi Wowote wa Kero.

Lupyana Fute ni Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Anakiri Kupokea Malalamiko Hayo na Kusema Kuwa Tayari Halmashauri ya Mji wa Njombe Imeshayaingia Katika Mpango Wake wa Kuyafanyia Ukarabati

Akiwa Katika Mkutano wa Wamiliki na Madereva wa Vyombo Vya Usafiri Mjini Njombe,Mhandisi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw Peter Kawogo Anatumia Hadhara Hiyo Kuelezea Mipango ya Serikali Katika Kutatua Kero Hiyo.

0 comments:

Post a Comment