tg

Friday, February 28, 2014

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DKT TITUS KAMANI AMEZINDUA KITUO CHA KUKUSANYIA,KUHIFADHI NA KUPOOZA MAZIWA KATA YA MTWANGO NJOMBE.





Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani Amezindua Kituo Chenye Tanki la Kukusanya , Kupoza na  Kuhifadhi Maziwa Lenye Thamani ya Shilingi Milioni 20 Katika Kijiji cha Wangama Wilayani Njombe Kilichopo Chini ya Mtandao wa Vikundi Vya Wafugaji, Pamoja na Kuwatembelea Wafugaji wa Ng'ombe Katika Kijiji cha Ibumila .

Akiongea Mara Baada ya Kuzindua Kituo Hicho Dkt. Kamani Amesema Kuwa Serikali Inatarajia Kutoa Ng'ombe Elfu 40 wa Maziwa na Kuwagawa Katika Wilaya za Mkoa wa Njombe Likiwemo Shamba la Kitulo Wilayani Makete Ikiwa ni Hatua ya Kuendelea Kuwaunga Mkono Wafugaji Mkoani  Hapa.

Waziri Huyo wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Amesema Serikali Imeanza Maandalizi ya Kuanzisha Kituo Maalum Kwa Ukanda wa Nyanda za Juu Kitakacho Kuwa Sao Hill Ili Kupata Mbegu Bora za Ng'ombe wa Maziwa , Huku Akiziagiza Halmashauri na Mamlaka za Mkoa Kusaidia Kufuatilia Wawekezaji Binafsi Katika Uhamasishaji.

Keptain Mstaafu Aseri Msangi ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ambaye Amesema Changamoto Kubwa Inayowakabili Wafugaji ni Ukosefu wa Mbegu Bora za Ng'ombe wa Maziwa na Kumuomba Waziri Huyo Kuwasaidia Wafugaji Kupata Mbegu Hizo Bora za Ng'ombe wa Maziwa Huku Akiwataka Wafugaji Kuwatunza Ng'ombe Wao Kwa Kuwapa Chakula cha Kutosha Ili Kupata Maziwa Mengi.

Katika Risala Fupi Iliyosomwa Kwaniaba ya Wafugaji wa Kutoka Vijiji 11 Vya Wafugaji Wilayani Njombe Imeeleza Kuwa Vijiji Vya Mtandao wa Wafugaji Vina Jumla ya Ng'ombe wa Maziwa Mia 669  na Kwamba Kati ya Hao Huzalisha Wastani wa Lita Elfu 2664 za Maziwa Kwa Siku.

0 comments:

Post a Comment