Tabia
ya wakazi wengi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe kujenga vyoo vidogo
kiasi cha watumiaji kupata shida kuingia kujisaidia, imemchefua mkuu wa
mkoa huo wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo hivi karibuni
Akizungumza
wilayani hapa mkuu wa mkoa wa Njombe Kapt. Aseri Msangi amesema
anakerwa na tabia ya wananchi wa makete wanaojenga vyoo vidogo hali
inayosababisha kero kwa watumiaji kutokana na kupata shida tangu
anapoingia hadi kutoka
"Mimi
nashangaa kabisa badala ya mtu kujenga choo kikubwa kitakachopelekea
mtu kujisikia nafuu anapoingia kujisaidia nyie mnajenga choo ambacho mtu
akiingia kwanza anainama, na pili hawezi kugeuka akiingia, yaani
akiingia kwa mbele anarudi kinyume nyume" alisema Msangi
Ametoa
wito kwa wananchi hao kujenga vyoo vikubwa na vyenye ubora kwani kwa
kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza magonjwa ya matumbo
ambayo yanawakumba wananchi wengi na uchunguzi kubaini kuwa ni kutokana
na kukosekana kwa vyoo bora vinavyotunzwa vizurI
NA eDDy bLOG
0 comments:
Post a Comment