tg

Monday, February 24, 2014

MICHANGO YA MADAWATI SHULENI MARUFUKU NJOMBE


 Wananchi na Wafuasi wa CHADEMA Wakimpokea Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Katika Geti Lililopo Ramadhani Kwa ajili ya Ufunguzi wa Tawi la CHADEMA.


 Mwakilishi Toka Chadema Taifa Emmanuel Masonga Akizungumza na Wakazi wa Mtaa wa Ramadhani Jana

 Hapa Diwani Mtambo Akizindua Ofisi ya Chadema Tawi la Ramadhani
Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Agrey Mtambo Akizungumza na Wakazi wa Mtaa wa Ramadhani Mjini Njombe Hapo Jana

Na Gabriel Kilamlya

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kata ya Njombe Mjini Kupitia Diwani Wake Kimeanza Kutoa Matamko Mbalimbali Kupitia Diwani wa Kata Hiyo Bwana Agrey Mtambo.

Miongoni Mwa Matamko Yaliyoanza Kutolewa ni Pamoja na Kuruhusu Wananchi Kuanza Kulima Kwenye Mito na Si Kwenye Vyanzo Vya Maji.

Aidha Diwani Mtambo Amesema Kuwa Kuanzia Sasa Serikali Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Imetangaza Kutochangia Michango ya Madawati kwa Wanafunzi Shuleni.

Matamko Hayo Yalianza Kutolewa Wakati wa Ufunguzi wa Tawi la CHAMA Hicho Tawi la Ramadhani na Kumalizi Katika Mkutano Mkubwa Katika Mtaa wa National Housing Mjini Njombe.

0 comments:

Post a Comment