tg

Sunday, July 28, 2013

ZAHANATI YA KIJIJI CHA IKONDO WILAYANI NJOMBE IMEFUNGWA KUTOKANA NA WAUGUZI KWENDA KWENYE SEMINA ....






 TAARIFA YA KATA YA IKONDO ILIYOSOMWA NA AFISA MTENDAJI WA KATA HIYO







Zahanati ya Kijiji cha Ikondo katika kata ya Ikonda wilayani Njombe ilisimama kufanya kazi kwa muda wa siku ya mbili baada ya wauguzi na wakunga wa zahanati hiyo kufunga na kwenda kwenye semina mjini Njombe ambapo pamoja na mambo mengine wagonjwa wa kijiji hichowalikuwa hatarini kupoteza maisha kwa kukosa huduma za matibabu.

Wakizungumza Mbele ya Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Bwana Deo Sanga wananchi wa kijiji cha Ikondo walilalamikia kufungwa kwa zahanati hiyo kutokana na kile kilicho daiwa kuwa madaktari walikwenda kwenye semina ya tarehe  23 na 24  huku wagonjwa wakiachwa pasipo kupatiwa huduma za matibabu.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa katika zahanati hiyo wanakabiliwa na changamoto mbali,mbali ikiwemo ya ukosefu wa nyumba za waganga,ukosefu wa dawa zikiwemo za kuvubaza makali ya virusi vya UKIMWI na kwamba kwa sasa wanasafiri umbali wa zaidi ya kilomita 50 kwenda kupata tiba hiyo kutokana na zahanati hiyo kuwa haina uwezo wa kutoa huduma hiyo.
 
Akizungumzia tatizo la kufungwa kwa zahanati hiyo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Filbert Mbwiro amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha kufungwa kwa zahanati hiyo na kwamba ni kinyume cha sheria kwa watumishi wa afya kufunga zahanati na kuondoka wote kuelekea kwenye semina na kwamba atalifuatilia halmashauri kujua aliyetoa barua ya kwenda kwenye semina kwa watumishi na kufunga zahanati hiyo.

Aidha bwana Mbwiro amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watumishi hao mara tu itakapobainika wameondoka pasipo utaratibu nakuwataka radhi wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki wakati  taratibu za kuwatafuta wauguzi hao ili kuendelea kutoa huduma zikiendelea katika zahanati hiyo.

Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini bwana Deo Sanga amemuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kuhakikisha zahanati hiyo inafunguliwa mapema iwezekanavyo na kwamba watumishi

0 comments:

Post a Comment