tg

Sunday, July 28, 2013

KESI YA DIWANI WA KATA YA RAMADHANI IMEENDELEA KUPIGWA KALENDA NJOMBE.

Diwani wa Kata ya Ramadhani Bwana Alfred Luvanda  Ambaye Alishambuliwa na Kujeruhiwa na Katibu Mwenezi wa Kata Hiyo Bwana Erasto Ngole.

Kesi ya Kushambulia na Kumjeruhi Diwani wa Kata ya Raamadhani Alfred Luvanda Inayomkabili Katibu Mwenezi wa CCM kata ya Ramadhani Erasto Ngole Imeendelea Kuahirishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe kwa Kumkosa Shahidi wa Upande wa Mashtaka.

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama Hiyo Bwana Serapian Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa Shahidi wa Upande wa Mashtaka ambaye ni Dokta wa Hospitali ya Muhimbili ambaye alikuwa akimtibu Majeruhi Alfred Luvanda ameshindwa Kufika Mahakamani hapo.

Kwa mara Nyingine Tena Kesi Hiyo Imeahirishwa kwa Kumkosa Shahidi huyo ambapo awali Kesi hiyo Iliahirishwa Kutokana na
Shahidi Huyo kushindwa Kufika Mahakamani.

Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Ameahirisha Kesi hiyo Hadi Agosti 22 Mwaka Huu shahidi atakapofika Mahakamani Hapo.

0 comments:

Post a Comment